Man United kuwauza wachezaji saba Januari 2022

Muhtasari
  • Man United kuwauza wachezaji saba Januari 2022
  • Klabu hiyo pia itawakopesha wachezaji wa juu kwa vilabu vya juu ili kuboresha ujuzi wao
elazalkmaarmanutd031019
elazalkmaarmanutd031019

Manchester United wanajiandaa kuwauza wachezaji wake saba mwezi Januari 2022, ikiwa dirisha la uhamisho wa wachezaji Ulaya likafunguliwa.

United imekusanya wachezaji wengi sana hivi kwamba inabidi wawachilie wengine, vinginevyo kulipa mishahara kunaweza kuwaingiza katika changamoto ya kiuchumi.

Kulingana na gazeti The Sun, United litawauza wachezaji Donny van de Beek, Jesse Lingard, Phil Jones, Eric Bailly, Anthony Martial, Diogo Dalot na Alex Telles.

Klabu hiyo pia itawakopesha wachezaji wa juu kwa vilabu vya juu ili kuboresha ujuzi wao.

Lakini, United inajitahidi kumshawishi Paul Pogba abaki Old Trafford, huku mkataba wake ukimalizika mwishoni mwa msimu ujao.

Pogba ananyatiwa na vilabu kadhaa ikiwemo klabu yake ya zamani Juventus, Real Madrid na Paris St Germain, kulingana na ripoti.

Hata hivyo kujumuishwa kwa jina la Jesse Lingard kwenye orodha ya uhamisho ya United mnamo Januari ni hatua ya kushangaza baada ya Ole Gunnar Solskjaer kudokeza kuwa anataka mchezaji huyo wa kimataifa wa England abaki Old Trafford.