Newcastle yampiga kalamu kocha mkuu Steve Bruce

Muhtasari

•Klabu ya Newcastle ambayo kwa sasa  imekalia nafasi ya 19 katika jedwali la EPL imetangaza kwamba harakati ya kutafuta kocha mpya imeng'oa nanga.

•Haya yanajiri siku chache tu baada ya klabu hiyo kupata wamiliki wapya kutoka Saudia wanaoaminika kuwa mabwenyenye wakubwa kweli.

Steve Bruce
Steve Bruce
Image: NEWCASTLE WEB

Steve Bruce ameacha nafasi yake kama kocha mkuu wa klabu ya Newcastle.

Klabu hiyo ya EPL imetangaza kwamba Bruce amoeondoka kufuatia maafikiano ya pamoja.

Bruce ambaye ana umri wa miaka 60 ameondoka Newcastle baada ya kuhudumu kama kocha kwa kipindi cha takriban miaka miwili.

Klabu ya Newcastle ambayo kwa sasa  imekalia nafasi ya 19 katika jedwali la EPL imetangaza kwamba harakati ya kutafuta kocha mpya imeng'oa nanga.

"Harakati ya kutafuta kocha mkuu mpya imeanza na uteuzi utatangazwa kwa wakati. Klabu haitakuwa inatoa taarifa zaidi kwa sasa" Newcastle ilitangaza kupitia tovuti yake rasmi.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya klabu hiyo kupata wamiliki wapya kutoka Saudia wanaoaminika kuwa mabwenyenye wakubwa kweli.