Europa League: Matokeo ya raundi ya 3 kwenye hatua ya makundi, Hali ilivyo kwenye jedwali

Muhtasari

•Kwa sasa Lyon inaongoza kundi A, Monaco iko kileleni katika kundi B, Legia Warsaw  inaongoza kundi C, Frankfurt kundi D, Galatasary inatawala kundi E, Crvena Zvezda iko kileleni katika kundi F, Bayer Leverkusen wanaongoza kundi G huku Westham wakiwa bora katika kundi H.

Image: EUROPA LEAGUE

Michuano ya Europa League iliingia katika raundi ya tatu usiku wa Alhamisi huku jumla ya mechi 14  zikichezwa katika nchi mbalimbali bara Ulaya.

Mechi sita za kwanza zilichezwa mwendo wa saa mbili kasorobo ambapo nne kati yazo ziliishia sare.

Fernebache walitoka sare ya 2-2 dhidi ya Antwerp ya Ubelgiji,Real Betis wakatoka sare ya 1-1 na Bayer Leverkusen , Midjylland ya Denmark vile vile wakatoka sare ya 1-1 na Crvena Zvezda ya Serbia  huku mechi kati ya Lazio na Marseille ikiangulia sare tasa.

Sporting Braga ya Ureno iliweza kupata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Ludogorets huku Rapid Vienna ikishinda Dinamo Zagreb ya Croatia 2-1 nyumbani.

Mechi nane za kusisimua zilichezwa mida ya saa nne usiku .

 Wawakilishaji  wa EPL West Ham United waliweza kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Genk ya Ubelgiji siku moja tu baada ya wenzao Leicester kushinda Spartak Moscow ya Urusi 4-3 ugenini.

Napoli iliweza kushinda Legia Warsaw 3-0, Lokomotiv Mosscow ikapoteza 0-1 nyumbani dhidi ya Galatasary, Rangers ikashinda 2-0 nyumbani dhidi ya Brondby ya Denmark. Eintracht Frankfurt wakapata ushindi wa 3-1 dhidi ya Olympiacos Piraeus huku Lyon na Real Sociedad zikipata ushindi wa 4-3 na 1-0 dhidi ya Sparta Prague na Sturm Graz mtawalia licha ya wachezaji wao wawili kupewa kadi nyekundu.

Kwa sasa Lyon inaongoza kundi A, Monaco iko kileleni katika kundi B, Legia Warsaw  inaongoza kundi C, Frankfurt kundi D, Galatasary inatawala kundi E, Crvena Zvezda iko kileleni katika kundi F, Bayer Leverkusen wanaongoza kundi G huku Westham wakiwa bora katika kundi H.