Patrice Evra: Mlinzi wa zamani wa Manchester United asema alinyanyaswa kingono katika umri wa kubalehe

Muhtasari

•Evra, ambaye alikulia katika kitongoji cha Les Ulis karibu na jiji la Paris, anasema unyanyasaji huo dhidi yake ulifanyika katika nyumba ya mwalimu, ambako aliiishi ili kupunguza muda wa usafiri baina ya nyumbani kwao na shuleni.

•Evra anasema alikanusha unyanyasaji wakati alipopokea simu kutoka kwa polisi kuhusiana na unyanyasaji huo, alipokuwa akichezea klabu ya Monaco akiwa na umri wa miaka 24.

Image: GETTY IMAGES

Mchezaji wa zamani wa safu ya ulinzi wa zamani wa Manchester Patrice Evra says anasema alinyanyaswa kingono na mwalimu wake alipokuwa katika umri wa kubalehe.

Evra, mwenye umri wa miaka 40 kwasasa, alizungumzia hilo wazi katika mahojiano na gazeti la The Times la Uingereza kabla ya kutoa kitabu chake.

Alielezea ni kwanini hakuwahi kuzungumzia suala hilo hadi sasa.

"Kwanza nilipoandika kitabu, sikuelezea hadithi yote kwa sababu nilikuwa nina aibu na kuogopa ni nini watu wangefikiria ," alisema Evra.

"Sasa ninataka kusema kwasababu sitaki watoto wawe katika hali yangu na kuhisi kuaibika, wakifikiria kwamba hawana ujasiri, ni sual la utayari wa akili wa kuzungumzia suala hili.

"Kwahiyio ninataka kuwafanya watoto wawe na ujasiri na wasijilaumu wenyewe, kwasababu kila mara nimekuwa nikijilaumu mwenyewe.

"Sina aibu ya kusema kuwa nilihisi kama muoga kwa miaka mingi kwasababu sikuwahi kuzungumzia unyanyasaji huu wazi.Kilikuwa ni kitu kizito kifuani mwangu.Lakini sikukifanya mwenyewe. Ninafanya kwa ajili ya watoto wengine."

Evra, ambaye alikulia katika kitongoji cha Les Ulis karibu na jiji la Paris, anasema unyanyasaji huo dhidi yake ulifanyika katika nyumba ya mwalimu, ambako aliiishi ili kupunguza muda wa usafiri baina ya nyumbani kwao na shuleni.

Alimwambia tu mama yake wiki mbili zilizopita, na akasema alikataa ombo la mama yake ambaye alimuomba asijadili jambo hilo katika kitabu.

"Ni sasa wakati nina umri wa miaka 40 ndio nimemwambia mama yangu," alisema. "Ulikuwa ni mshituko mkubwa kwake. Alikasirika sana. Aliniambia pole. Alisema, 'Usiweke hili katika kitabu chako, Ni jambo la kibiafsi'.

"Lakini hapo ndipo niliposema, 'Mama, sio kuhusu mimi, ni kuhusu watoto wengine, halafu akaniambia SAWA, anaelewa."

Image: GETTY IMAGES

Evra, ambaye alishinda mataji matano ya Primia Ligi katika kipindi cha miaka minane alichokuwa katika Old Trafford,anasema alikanusha unyanyasaji wakati alipopokea simu kutoka kwa polisi kuhusiana na unyanyasaji huo, alipokuwa akichezea klabu ya Monaco akiwa na umri wa miaka 24.

"Kuishi na kumbu kumbu ya unyanyasaji huu ni majuto makubwa sana kwasababu ningekuwa nimewasaidia watu wengi sana ," aliongeza.