Manchester United: Solskjaer hafukuziki Old Trafford?

Muhtasari
  • Wachezaji wengi wa zamani wa timu hiyo, wengine wamewahi kucheza na Solskjaer waasema muda umefika wa kocha huyo kuondoka
Image: BBC

Kipigo cha aibu cha mabao 5-0 ilichopata Manchester United kutoka Liverpool katika uwanja wa Old Trafford kumeleta maneno na shutuma dhidi ya kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer.

Mashabiki wengi wanaamini kwamba Mnorway huyo anapaswa kufungashiwa virago haraka baada ya kipigo kibaya zaidi cha nyumbani kutoka kwa wapinzani wao hao, ikiipiku kipigo walichowahi kukipata cha mabao 7-1 huko Liverpool mwaka 1895, wakati huo klabu hiyo inaitwa Newton Heath.

Wachezaji wengi wa zamani wa timu hiyo, wengine wamewahi kucheza na Solskjaer waasema muda umefika wa kocha huyo kuondoka.

Manchester kumfuta kazi Solskjaer?

Inavyoonekana sasa, kama atapewa muda wa kuendelea kukibeba kikosi hicho katika michezo kadhaa ijayo. Lakini hilo halimpi tiketi ya kujiona yuko salama kwneye kiti hicho. David Moyes na Jose Mourinho wwalifukuzwa baada ya vipigo walivyowahi kupata Jumapili wakiiongoza Manchester United. Moyes yeye baada ya kipigo cha ugenini cha mabao 2-0 kutoka kwa Everton, kipigo kilichomaanisha timu hiyo haitamaliza katika nafasi nne za juu, alitimuliwa.

Kwa upande wa Mourinho, kipigo kibaya cha 3-1 dhidi ya Liverpool kilimaanisha kwamba ilikuwa mechi yake ya mwisho kukinoa kisosi cha Manchester. Wote walitimuliwa baada ya Jumanne.

Mabosi wa United kwa miezi kadhaa wamekuwa wakisema Solskjaer anaipeleka klabu hiyo kwneye njia sahihi. Msimu uiopita kocha huyo alisaini mkataba mpya wa miaka 3, Msaidizi wake, Mike Phelan, alipewa mkataba mapema mwezi huu na mazungumzo yanaendelea kuwaongezea mkataba makocha wengine wa bechi lake, Michael Carrick na Kieran McKenna.

Hata kama atasalia kwenye kiti hicho sasa, je atapona katika michezo ijayo ambayo ni migumu? Katika michezo mine ijayo Manchester watacheza ugenini wiki ijayo dhidi ya Tottenham, baadae Manchester City, watakutana na Chelsea na Watford.

Kama amepata alama moja katika michezo minne iliyopita, ni ngumu kuvumilika akipoteza alama zingine dhidhi ya vigogo hao. Pengine anaweza kupata alama dhidi ya Watford, lakini ni mtihani mgumu kupata ushindi dhidi ya Spurs, City na Chelsea.

Man kwa sasa iko nafasi ya 7 ikiwa na alama 14. Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Ed Woodward anazungumza na familia ya Glazer wanaomiliki timu hiyo karibu kila siku. Mkurgenzi mkuu Richard Arnold, anatarajiwa kurithi mikoba ya Woodward atakapoondoka mwishoni mwa mwaka huu, pia amekuwa kwenye mawasiliao ya mara kwa mara na wamiliki. Hilo linaongeza wasiwasi wa nafasi ya Ole.

Wachezaji wana mtazamo gani?

BBC inafahamu kwamba idadi ya wachezaji waliopoteza imani na Solskjaer inazidi kuongezeka. Hawaamini mbinu zake na wanadhani uwezo wake ni mdogo ukilinganisha na makocha wengine wa klabu kubwa kama Pep Guardiola, Jurgen Klopp na Thomas Tuchel.

Hii inaonekana kama vile wachezaji wanataka kukwepa wajibu wao na kumsukumia mzigo Ole. Hata hivyo wachezaji wa zamani pia wamekosoa mbinu za Solskjaer na kushutumu namna timu yake ilivyocheza dhidi ya Liverpool.

Baada ya ushindi dhidi ya Atalanta Jumatano walipokuwa nyuma kwa mabao 2-0 mpaka kipindi cha kwanza kinaalizaka- kiungo wa zamani wa United Paul Scholes alisema alihofia nini kitatokea dhidi ya Liverpool kama watachezaji walivyokuwa wanacheza.

Bahati mbaya kwao, wakachezaji hivyo hivyo wakiwa na kikosi kile kile dhidi ya Liverpool na kufungwa kwa aibu.

Kama atatimuliwa, nani kurithi mikoba yake?

Uamuzi wa kumtimu ni rahisi kuliko kupata mbadala wake. Wengi wanasema uamuzi wa Manchester United wa kuendelea kumpa muda kidogo kama itathibitishwa hivyo, umeangalia ugumu wa kumpata mrithi wake.

Lakini uamuzi mwingine rahisi na kumbakiza Solskjaer aendelee na majukumu yake, kitu ambacho kinapingwa na mashabiki wengi waliochoshwa nae. Hata wakati huo, mashabiki hawakufurahishwa na mwenendo wa makocha wake, lakini United waliendelea kuwa nao, mfano Moyes, Louis van Gaal na Mourinho waliendelea kukalia viti vyao kwa muda mrefu licha ya makelele ya kutimuiwa haraka kutoka kwa mashabiki.

Vinasaba vya Manchester vinampa nafasi mpaka leo Ole kusalia pale, akiwa mmoja wa wachezjai walioleta mafanikio kwenye klabu hiyo, akionekana ni mwenzao, mwenye damu ya timu hiyo na mshabiki mkubwa. Lakini mashabiki wanataza furaha ya sasa wakiona ni wakati wa kocha mpya kurithi mikoba yake.

Majina mawili makubwa yanayotajwa sasa ni kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte na meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane.

Conte anaonekana kama hana nafasi kutokana na kwenda tofauti na mtazamo wa viongozi wa juu wa United., lakii mafanikio yake ya msimu uliopita yaliyoipa Inter Milan taji la ligi kuu ya Italia 'Seria A, yanamfanya kuwa kwneye nafasi ya kufikiriwa.

Zidane alishinda makombe mengi Real Madrid, licha ya wasiwasi wa kukaa kwenye mechi kufundisha, igawa makocha kama Klopp na Guardiola wamekuwa wakimsifu kwa uwezo wake wa kuboresha viwanngo vya wachezaji.

Mfaransa huyo hana timu toka aondoke Madrid mwezi Mei. Hana uzoefu w aligi kuu Uingereza na hazungumzi Kiingereza hilo linaleta ukakasi wa kupewa nafasi - ingawa yuko kocha wa Leeds Marcelo Bielsa ambaye ameonyesha lugha sio tatizo .

Ukiacha makocha hao, yuko kocha wa Ajax Eric ten Hag ambaye alikataa kuondoka katikati ya msimu alipotakiwa kujiunga na Bayern Munich mwaka 2019,.

Yote yanaleta ugumu wa kumuondoa haraka Ole.