Jesse Lingard: Hali ya baadaye ya kiungo wa kati wa Man Utd mashakani

Muhtasari

•Lingard aliamua kubakia Manchester United msimu huu licha ya kwamba klabu sita zilikuwa zinamtaka, akiamini kuwa meneja Ole Gunnar Solskjaer angempatia muda zaidi wa mechi.

Image: GETTY IMAGES

Hali ya baadaye ya Jesse Lingard katika Manchester United iko mashakani baada ya kuvunjika kwa mazungumzo mapya kuhusu mkataba wake.

Mkataba wa Lingard mwenye umri wa miaka 28- unamalizika msimu ujao na Manchester United walikuwa na matumaini ya kurefusha muda zaidi wa kiungo huyo wa kati wa England katika Old Trafford kufuatia mkataba mzuri wa mkopo katika West Ham katika kipindi cha nusu ya msimu uliopita.

Lingard aliamua kubakia Manchester United msimu huu licha ya kwamba klabu sita zilikuwa zinamtaka, akiamini kuwa meneja Ole Gunnar Solskjaer angempatia muda zaidi wa mechi.

Badala yake, Lingard amecheza mechi moja tu msimu mzima , wa kombe la EFL ambapo walishindwa na West Ham katika mwezi wa Septemba. Pia alikuwa miongoni mwa wachezaji wa ziada mara saba, kwa ujumla dakika 76. Hii inamaanisha kuwa amekuwa namuda wa zaidi ya mechi moja kwa ajili ya England wakati wa mechi kuliko katika United, ingawa alipoteza nafasi yake katika kikosi chaGareth Southgate cha washindi waliofuzu kwa Kombe la dunia dhidi ya Albania na San Marino.

Lingardni mmoja wa wachezaji kadhaa ambao wamebaki na mkanganyiko kutokana na uamuzi wa Solskjaer wa kutowapatia wachezaji zaidi fursa huku klabu hiyo ikitaka kujikwamua kutokana na matokeo mabaya, ikiwa ni pamoja na kipigo cha Liverpool cha mabao 5-0, waliyofungwa nyumbani na mabao 2-0 waliyofungwa na Manchester City.

Manchester United inacheza na Watford katika mchezo wa Primia Ligi Jumamosi,, Villarreal katika mchezo wa Championi Ligi Jumanne na itacheza na Chelsea Jumapili tarehe 28 , Novemba.

Inafahamika kwamba katika hali aliyonayo, Lingard, ambaye amekuwa katika Machester United tangu alipokuwa na umri wa miaka saba, haoni sababu ya kufanya mazungumzo zaidi na atakuwa na matumaini ya kupata mkataba wa mkopo wa uhamisho katika mwezi Januari.