Manchester United wamemuajiri Ralf Rangnick kuwa mkufunzi wake wa muda

Muhtasari
  • Iwapo kitachelewa , Mkufunzi wa muda huu Michel Carrick atasalia kuinoa klabu hiyo
  • Kikosi hicho kimejaa talanta na kina wachezaji vijana na wale walio na uzoefu alisema Rangnick

Manchester United wamemuajiri Ralf Rangnick kuwa mkufunzi wa muda hadi mwisho wa msimu huu .

Raia huyo mwenye umri wa miaka 63 anamrithi mtangulizi wake Ole Gunnar Solskjaer ambaye alifutwa kazi Novemba 21 baada ya kulazwa 4-1 na klabu ya Watford.

Rangnick amewacha kazi yake kama mkuu wa michezo na maendeleo katika klabu ya Lokomotiv Moscow ili kuchukua kazi hiyo.

'Ninafurahi kujiunga na Man United kufanikisha msimu huu , alisema Rangnick''.

Kufuatia kukamilika kwa msimu huu , Rangnick atasalia katika uwanja wa Old Trafford kwa miaka miwili kama mshauri.

Mechi yake ya kwanza akisimamia United , ambao wako katika nafasi ya nane katika ligi ya Premia huenda ikawa dhidi ya Arsenal tarehe 2 Disemba iwapo cheti chake cha kufanya kazi kitapatikana mapema.

Iwapo kitachelewa , Mkufunzi wa muda huu Michel Carrick atasalia kuinoa klabu hiyo.

Kikosi hicho kimejaa talanta na kina wachezaji vijana na wale walio na uzoefu alisema Rangnick.

Juhudi zangu zote katika kipindi cha miezi sita itakuwa kusaidia wachezaji hawa kuonesha vipaji vyao kibinafsi na kama timu