Arsenal yampokonya unahodha wa timu Pierre Emerick Aubameyang

Muhtasari
  • Arsenal yampokonya unahodha wa timu Pierre Emerick Aubameyang
Pierre Emerick Aubameyang
Image: Hisani

Arsenal wamempokonya unahodha wa timu hiyo mashambuliaji wao Pierre Emrick Aubameyang baada ya kukosa nidhamu.

Mshambuliaji huyo wa Gabon , ambaye hakushirikishwa katika mechi ya Jumamosi ambayo Arsenal ilishinda 3-0 dhidi ya Suthampton , pia hatoshirikishwa katika mechi dhidi ya West Ham siku ya Jumatano.

''Tunataraji wachezaji wetu wote hususan nahodha wetu , kufuata sheria na viwango vilivyowekwa na kukubalika'', ilisema taarifa ya Arsenal.

Aubameyang, 32, aliwachwa nje kwa makosa ya kinidhamu mnamo mwezi Machi.

Pia imesea kwambahatashirikishwa katika mchuano wa jumatano ambao watachuana na West Ham United.

Hivi karibuni Aubameyang hajakuwa na matokea ya kuridhisha kwa mashambiki wa Arsenal ambao wameonekana kutofurahia mchezo wake.

Arsenal imewaeleza wachezaji wote ikiwemo na nahodha, wafuatilie maagizo ambayo yamewekwa na wajiadae kwa mechi inayokuja.

Aubemayang mwenye umri wa miaka 32, msimu huu ameweza kufunga mabao 4 pekee.

Jambo ambalo linachukuliwa na wachanganuzi wa soka kuwa mchezo wake umeshuka kwa kiwango kikubwa ukiringanisha na misimu ya hapo nyuma