Mechi kati ya Brentford na United yaahirishwa kufuatia kuzuka kwa COVID-19 Old Trafford

Muhtasari

•Siku ya Jumatatu Manchester walifunga uwanja wa Carrington kufuatia visa vya Covid  19 vilivyoripotiwa  kwenye kambi lao

Image: MANUTD.COM

Mechi  kati ya  Machester united na Brentford imeahirishwa kufuatia kusambaa kwa Corona kwenye kambi la manchester united.

Kupitia mtandao wa Twitter Manchester united wamesema ligi kuu ya Uingereza imekubali kusitisha mechi yao na Brentford iliyotarajiwa kuchezwa usiku wa Jumanne kati yao na Bentford.

Siku ya Jumatatu Manchester walifunga uwanja wa Carrington kufuatia visa vya Covid  19 vilivyoripotiwa  kwenye kambi lao. Hii ni baada ya wafanyakazi  kadhaa kupimwa na kupatikana na virusi hivo.

Kufuatia hayo klabu iliwandikia EPL  barua ikieleza jinsi hali ilivyo katika uwanja wao.

EPL  ilikubali ombi lao na kuahirisha mechi hadi wakati usiodhibitishwa.

Hivi karibuni visa vya Corona vimeripotiwa kuongezeka katika nchi ya  Uingereza na kusababisha kuahirishwa kwa mechi kadhaa.

Timu ambazo zimeadhiriwa zaidi na virusi hivo ni Tottenham, Brighton na hivi karibuni machester imetangaza kuadhiriwa pia.

Hofu kubwa kwaa sasa ni kwamba kufuaitia yanayojiri huenda EPL  ikapiga marufuku mashabiki kuhudhuria mechi  zitakazochezwa siku zijazo.