Benjamin Mendy: Mchezaji soka wa Man City ashtakiwa kwa ubakaji mwingine

Muhtasari
  • Mchezaji wa Manchester City Benjamin Mendy ameshtakiwa kwa kosa jingine la ubakaji
  • Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alishtakiwa wiki iliyopita kwa kosa la hivi punde lakini ilikuwa chini ya vikwazo vya kuripoti
Mwanakandanda Benjamin Mendy
Image: BBC

Mcheza

ji wa Manchester City Benjamin Mendy ameshtakiwa kwa kosa jingine la ubakaji

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, wa Prestbury huko Cheshire, sasa anatuhumiwa kwa makosa saba ya ubakaji na shtaka moja la unyanyasaji wa kijinsia unaohusiana na wanawake watano.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alishtakiwa wiki iliyopita kwa kosa la hivi punde lakini ilikuwa chini ya vikwazo vya kuripoti.

Vikwazo hivyo viliondolewa awali wakati Bw. Mendy alipowasili katika mahakamat Chester Crown kwa ajili ya kusikizwa kabla ya kesi.

Shtaka la hivi punde linahusiana na mlalamishi mpya na linadaiwa kufanyika Julai mwaka huu.

Makosa ya awali yanadaiwa kufanywa kati ya Oktoba 2020 na Agosti 2021.

Mwanasoka huyo, ambaye amekuwa kizuizini tangu kukamatwa kwake mwezi Agosti, alionekana pamoja na mshtakiwa mwenzake Louis Saha Matturie, 40, wa Eccles huko Greater Manchester.

Anashtakiwa kwa makosa sita ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kijinsia.

Wanaume wote wawili waliwekwa rumande katika HMP Altcourse huko Liverpool baada ya kusikilizwa kwa dakika 40.

Kesi yao, ambayo ilipangwa Januari, pia ilirejeshwa nyuma hadi baadaye mwaka huu.

Mendy amewachezea mabingwa wa Premier League msimu uliopita Manchester City tangu 2017, alipojiunga kutoka Monaco kwa kima cha £52m..