Wolves yaadhibu Man U Oldtraford

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo
Image: twitter/Man united

Mashabiki wa Machester united Jumatatu usiku walinyamazishwa kwa kichapo kilichowakosesha usingizi na timu limbukeni ya Wolves.

Machester United,  ilitimua kocha, Ole Gunner kutokana na msururu wa matokeo duni na kumkabidhi mikoba kocha  Mjerumani Ralf Rangnick.

Kocha huyo alipatana na kichapo chake cha kwanza siku  ya Jumatatu  kwenye uwanja wa Old Tralford.   

Manchester ilifungwa bao hilo la kipee  mnamo dakika  ya 82 kupitia mchezaji Joah Moutinho na juhudi za manchester united kujaribu kukomboa ziliambulia patupu. 

Wachezaji wa zamani walioichezea machester united, wengi wao  walionyesha hofu yao kupitia ukurusa wao wa twitter na kutilia shaka mwelekeo wa Mashetani hao wekundu 

Katika ukurusu wa twitter Gary  Neville alisema "Sio nzuri. Kweli sivyo!"

@Ben- "Haijalishi ni mabadiliko gani yanafanywa, matokeo na maonyesho ni sawa. Klabu hii haijakamilika. #MUFC"

bangster-@manutd #mufc takataka tena kabisa!

John Bennett @johnmbennett Hakuna anayepaswa kushtuka. Sisi ni klabu mbaya ya soka #MUFC

Kutoka ujio wa Kocha, Ralf Rangnick Man U imecheza mechi 5, kushinda mara nne  4 na kutoka sare mechi moja.

Ole Gunner alishinda mechi kwa miezi  mitatu mfululizo, Rekodi ambayo Ralf ameshindwa kuivunja kwa kuwa yake ameshinda mechi 5 pekee.