Arsenal yatozwa faini ya Sh3M kwa kukosa kudhibiti wachezaji wake

Muhtasari

•Klabu hiyo ya London imekiri makosa yake na kukubali adhabu ya kutoa faini ya pauni 20,000 kama ilivyopendekezwa.

Image: GETTY IMAGES

Shirikisho la soka (FA|) limetoza klabu ya Arsenal pauni 20,000 (Ksh 3M) baada ya kukabili kosa la kukosa kudhibiti wachezaji wake katika mechi dhidi ya Mancheter City siku ya Jumamosi.

FA ilikuwa imepatia Wanabunduki hadi Ijumaa kujibu mashtaka ya kushindwa kuhakikisha wachezaji wao wanajiendesha kwa utaratibu ufaao wakati wa mechi hiyo iliyochezwa ugani Emirates.

Tukio hilo lilitokea dakika ya 59 baada ya beki wa Gunners, Gabriel Magalhaes kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupokea kadi ya pili ya njano.

Kufuatia hayo klabu hiyo ya London imekiri makosa yake na kukubali adhabu ya kutoa faini ya pauni 20,000 kama ilivyopendekezwa.