Nigeria, Gabon zayaaga mashindano ya AFCON 2021

Muhtasari

•Nigeria imeyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 na Timu ya Tunisia.

•Licha ya timu hio kuwa na ubora wa aina yake kwenye hatua ya makundi ambapo walimaliza wakiongoza kwenye kundi lao na Kwa Pointi 9 bila kupoteza mechi yoyote.

•Gabon ilitangulia kufunga kupitia  Traole dakika ya 28 bao  ambalo lilisawasishwa dakika ya 91 na kupelekea mechi hio kwenda kwenye Matuta penati.

 

wachezaji wa Tunisia wakisherekea ushindi
wachezaji wa Tunisia wakisherekea ushindi
Image: twitter/ AFCON

Ni usiku ambao umekuwa mrefu kwa mashabiki wa Nigeria almaarufu Super Eagles kubanduliwa kwenye mashindano ya Kombe la mabingwa la Afrika(AFCON) .

Nigeria imeyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 na Timu ya Tunisia.

Licha ya timu hio kuwa na ubora wa aina yake kwenye hatua ya makundi ambapo walimaliza wakiongoza kwenye kundi lao na Kwa Pointi 9 bila kupoteza mechi yoyote.

Bao la Tunisia lilifungwa dakika ya 47 na Mchezaji wao Youssef Msakni na kuwapepeka robo fainali ya Michuano hio.

Nigeria walipata pigo zaidi baada ya mchezaji wao wa kati Alex Iwobi kuonyeshwa kadi nyekundu dakika chache baada kuingia kwenye mechi hio.

Kwenye mechi nyingine AFCON2021, Burkina Faso walibandua Gabon kupitia matuta ya penati 7-6.

Gabon ilitangulia kufunga kupitia  Traole dakika ya 28 bao  ambalo lilisawasishwa dakika ya 91 na kupelekea mechi hio kwenda kwenye Matuta penati.