Gor Mahia yavunja mkataba na kocha Mark Harrision

Muhtasari

• Vigogo vya mpira wa miguu nchini Kenya, Gor Mahia wametangaza kuvunja mkataba wa kocha mkuu pamoja na benchi la kiufundi la timu hiyo.

• Muingereza Mark Harrison, 60, alisaini mkataba na klabu ya Gor baada ya kocha wa awali Mreno Manuel Vaz Pinto kujitoa kama kocha wa timu hiyo kwa kile kilichoripotiwa kuwa ni maelewano ya pande zote husika.

Kocha Muingereza Mark Harrison
Image: Gor Mahia (Facebook)

Vigogo vya mpira wa miguu nchini Kenya, Gor Mahia wametangaza kuvunja mkataba wa kocha mkuu pamoja na benchi la kiufundi la timu hiyo.

katika habari iliyochapishwa kwenye kurasa zao mitandaoni Januari 29, klabu hiyo imetangaza kuwa baada ya tadhmini ndefu ya jinsi ambavyo klabu hiyo imekuwa ikifanya katika mechi za hivi karibuni, wamefikia mwafaka wa kukatisha mkataba wa kocha mkuu Muingereza Mark Harrison, pamoja na benchi la kiufundi wakiwemo kocha msaidizi Sammy Omollo "Pamzo" na mkufunzi wa walinda lango, Jerim Onyango.

Aidha, Gor Mahia imetangaza kwamba kwanzia sasa, Paul Nkata atachukua hatamu kama kocha wa mpito akisaidiwa na kocha wa timu ya vijana Jared Otieno huku mchakato wa kumtafuta kocha wa kudumu ukitarajiwa kuanza hivi karibuni.

klabu hiyo imemtakia Muingereza Harrison kila la kheri katika shughuli zake zingine katika tasnia ya kandanda.

ikumbukwe kuachishwa kazi kwa kocha Mark Harrison kumekuja miezi michache tu baada ya kupewa kandarasi na timu hiyo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka 2021 ambapo amekuwa akiiongoza Gor kwa miezi sita tu mpaka kufikia tarehe ya kukatishwa kwa kandarasi yake kama kocha.

Muingereza Mark Harrison, 60, alisaini mkataba na klabu ya Gor baada ya kocha wa awali Mreno Manuel Vaz Pinto kujitoa kama kocha wa timu hiyo kwa kile kilichoripotiwa kuwa ni maelewano ya pande zote husika.

Kabla ya kuja kwake Gor Mahia, kocha Harrison alikuwa tayari amehudumu kama kocha katika timu mbali mbali tajika vikiwemo vilabu vya Uingereza kama vile Southampton na Stoke City miongoni mwa timu nyingine zaidi ya kumi na tatu barani Afrika.

Kila la kheri kochi!