Mshambulizi wa United Mason Greenwood kuendelea kuzuiliwa kwa unyanyasaji wa kingono

Muhtasari

•Polisi wa Greater Manchester Police (GMP) walisema wamepewa muda zaidi wa kumhoji baada ya kuongezewa muda hapo awali hadi Jumatatu.

Mshambulizi wa United Mason Greenwood ashtumiwa kwa kosa la unyanyasaji wa kinyumbani
Mshambulizi wa United Mason Greenwood ashtumiwa kwa kosa la unyanyasaji wa kinyumbani
Image: HISANI

Mchezaji wa soka wa Manchester United Mason Greenwoodamekamatwa zaidi kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono na kutoa vitisho vya kuua.

Kiungo huyo wa miaka 20 alikamatwa kwa tuhuma za ubakaji na shambulio siku ya jumapili.

Polisi wa Greater Manchester Police (GMP) walisema wamepewa muda zaidi wa kumhoji baada ya kuongezewa muda hapo awali hadi Jumatatu.

Manchester United imesema hatachezea klabu hiyo hadi itakapotangazwa tena.

GMP ilisema mchezaji huyo alikamatwa siku ya Jumapili baada ya kikosi hicho "kufahamu kuhusu picha na video za mitandao ya kijamii zilizotshirikishwa na mwanamke akiripoti matukio ya kushambuliwa kimwili".

Ilisema hakimu aliwaongezea muda kwa mara ya pili kuendelea kumzuia hadi Jumatano.

ReutersCopyright: ReutersManchester United ilisema klabu hiyo "haikukubali vurugu za aina yoyote"Image caption: Manchester United ilisema klabu hiyo "haikukubali vurugu za aina yoyote"

Msemaji wa jeshi alisema uchunguzi unaendelea na mwanamke mmoja "anapewa usaidizi wa kitaalam".

Waundaji wa mchezo wa video EA Sports walisema Mshambuliaji huyo ameondolewa kwenye bidhaa za FIFA.