Tunaomba fainali ya AFCON isongeshwe mbele- Diaa al-Sayed

Muhtasari

• Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Misri, Diaa al-Sayed amewataka waandaaji wa mashindano ya AFCON kufikiria kuihamishia mechi ya fainali hadi siku ya Jumatatu badala ya Jumapili.

• Kwa mujibu wa Sayed, wapinzani wao, Senegal wamepata siku ya ziada ya kupumzika na kujiandaa.

Egypt National Football Team
Egypt National Football Team
Image: Instagram KWA HISANI

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Misri, Diaa al-Sayed amewataka waandaaji wa mashindano ya AFCON kufikiria kuihamishia mechi ya fainali hadi siku ya Jumatatu badala ya Jumapili.

Kwa mujibu wa Sayed, wapinzani wao, Senegal wamepata siku ya ziada ya kupumzika na kujiandaa.

''Ninataka kuwaeleza maafisa wote wa shirikisho la soka Afrika, CAF kwamba Senegal wamepata siku ya ziada ya kujianda, kwa hiyo, pengine mechi ya fainali ingehamishiwa Jumatatu,'' amesema kocha msaidizi wa Misri Diaa al-Sayed.

Senegal na Misri watashuka dimbani siku ya Jumapili kwenye fainali ya kufa mtu, huku Sadio Mane [Senegal] na Mohammed Salah [Misri] ambao kwa pamoja wanichezea Liverpool ya Uingereza wakitarajiwa kutoana jasho ili kujua nani ataibuka kidedea na kubeba taji la dimba hilo.