Hongera! Senegal wanyakua taji la kwanza la AFCON kwa kuibwaga Egypt

Muhtasari

•Mshambulizi matata wa Liverpool Sadio Mane ndiye alipigia Senegal penalti ya ushindi licha ya kushikiwa penalti nyingine hapo awali katika dakika ya saba ya mchezo.

Senegal wanyakua taji la kwanza la Afcon kwa kuibwaga Misri
Senegal wanyakua taji la kwanza la Afcon kwa kuibwaga Misri
Image: GETTY IMAGES

Mnamo usiku wa Jumapili 'Simba wa Teranga' walifanikisha ndoto yao ya kutwaa kombe la kwanza la Afcon baada ya kuishinda Misri katika fainali iliyochezewa ugani Yaoundé’s Olembe , Cameroon.

Fainali kati ya miamba hao wawili wa soka barani Afrika ambayo ilichezwa mwendo wa saa nne usiku iliishia sare tasa katika dakika za kawaida na za ziada hivyo kulazimu mikwanju ya penalti kuamua mshindi.

Senegal ilipoteza penalti moja tu huku Egypt ikipoteza mbili na kuiacha timu hiyo ya Afrika Magharibi kushinda kwa penalti 4-2.

Mshambulizi matata wa Liverpool Sadio Mane ndiye alipigia Senegal penalti ya ushindi licha ya kushikiwa penalti nyingine hapo awali katika dakika ya saba ya mchezo.

Ushindi huu ni afueni kubwa kwa Senegal ambao  hapo awali waliwahi kupoteza katika fainali mara mbili.

The Pharaohs hata hivyo bado wanaongoza kwenye orodha ya timu ambayo imewahi nyakua taji nyingi za Afcon huku ikiwa na saba tayari.