Wachezaji wa Senegal wazawadiwa dola 87,000 kila mmoja

Muhtasari

• Wachezaji wa timu ya taifa ya Senegal wamezawidia kima cha dola 87,000 na kipande cha shamba katika mji wa Dakar.

• Hili  limefanikishwa na rais wa taifa hilo, Macky Sall ambaye amesema  kwamba amechukua hatua hiyo kuwahongera wachezaji hao kwa kuiheshimisha nchi hiyo.

Senegal wanyakua taji la kwanza la Afcon kwa kuibwaga Misri
Senegal wanyakua taji la kwanza la Afcon kwa kuibwaga Misri
Image: GETTY IMAGES

Wachezaji wa timu ya taifa ya Senegal wamezawadiwa kima cha dola 87,000 na kipande cha ardhi katika mji wa Dakar baada ya kushinda taji la klabu bingwa barani Afrika nchini Cameroon.

Zawadi hizi zilifanikishwa na rais wa taifa hilo, Macky Sall ambaye amesema  kwamba amechukua hatua hiyo kuwahongera wachezaji hao kwa kuiheshimisha nchi hiyo.

Aidha rais Macky amemsifia kocha wa timu hiyo, Aliou Cisse kwa kuwaongoza vijana hao kwa utaalamu mkubwa uliopelekea wao kutawazwa mabingwa.

Ikumbukwe kwamba hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Senegal kushinda taji hilo tangu lianzishwe jambo ambalo limepelekea wananchi kusherehekea ushindi huo kwa ukubwa mno.

Hatua hii imeonekana kuwatia motisha wachezaji hao huku wengi wakisubiri kuona iwapo watatamba kwa hali sawa katika mashindano yajayo.