Kaka yake Kurt Zouma ajipata mashakani baada ya nduguye kumpiga paka

Muhtasari

•Zouma, 23, aliripotiwa kuchukua video ya mlinzi wa West Ham Kurt Zouma akimpiga teke na kofi mmoja wa wanyama wake wa nyumbani.

Yoan Zouma alikuwa mchezaji huru kabla ya kujiunga na Dagenham & Redbridge mnamo mwezi Desemba
Yoan Zouma alikuwa mchezaji huru kabla ya kujiunga na Dagenham & Redbridge mnamo mwezi Desemba
Image: Rex Features

Dagenham & Redbridge imesema Yoan Zouma hataichezea klabu hiyo hadi kukamilika kwa uchunguzi wa shirika la kufuatilia ustawi na kuzuia ukatili dhidi ya wanyama (RSPCA) kuhusu video ya kaka yake akimpiga teke paka.

Zouma, 23, aliripotiwa kuchukua video ya mlinzi wa West Ham Kurt Zouma akimpiga teke na kofi mmoja wa wanyama wake wa nyumbani.

Shirika la RSPCA tangu wakati huo limechukua paka wawili na wanawasiliana na Polisi wa Essex kuhusu tukio hilo.

Yoan Zouma alikuwa ameomba msamaha na kusema anajutia kuhusika kwake kwenye video hiyo.

Dagenham ilisema Zouma alitafutwa na shirika hilo wiki hii ili kusaidia katika uchunguzi wao na "alishirikiana nao kikamilifu."

Beki huyo wa kati wa Ufaransa alijiunga na timu ya Ligi ya Taifa mnamo mwezi Desemba na ameshiriki michuano sita.

"Dagenham & Redbridge FC ingependa tena kusisitiza kwamba inalaani aina yoyote ya ukatili dhidi ya wanyama na inaelewa kikamilifu hisia za wafuasi wake wengi," taarifa ya klabu ilisema.

"Kwa hivyo klabu imeamua kwamba hadi shirika la RSPCA likamilishe uchunguzi wake, Yoan hataichezea Dagenham & Redbridge katika mechi yoyote ile. "Hatua zaidi itakayoonekana inafaa kuchukuliwa itachukuliwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa RSPCA."

Kurt Zouma alitajwa katika kikosi cha kwanza cha West Ham dhidi ya Watford siku ya Jumanne, siku moja baada ya video hiyo kubainika.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipigwa faini ya "kiasi cha juu iwezekanavyov na West Ham siku ya Jumatano, na ada hiyo itapelekwa kwa mashirika ya kutoa misaada ya ustawi wa wanyama.