Je, Vinicius Junior wa Real Madrid kumpiku Neymar kama mshambuliaji bora wa Brazil?

Muhtasari

• Neymar ilibidi afafanue, akiilaumu DAZN kwa madai ya kuandika maoni nje ya muktadha.

Vinicius Junior (left) and Neymar (right) celebrate a goal for Brazil against Colombia in November
Vinicius Junior (left) and Neymar (right) celebrate a goal for Brazil against Colombia in November
Image: GETTY IMAGES

Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain Leonardo aliposikia tu taarifa hiyo, alichukua simu yake na kumpigia Neymar mara moja.

Kama ilivyo kwa kila mtu, Leonardo alishangaa aliposikia kupitia mahojiano yaliyorushwa na DAZN mwezi Oktoba mwaka jana kwamba nyota wake mwenye thamani ya euro milioni 222 anasema fainali za Kombe la Dunia la mwaka huu ni kama fainali "zake za mwisho", akisema hajui kama ana "nguvu na akili ya kupambana tena kwenye soka".

Haraka haraka Neymar ilibidi afafanue, akiilaumu DAZN kwa madai ya kuandika maoni nje ya muktadha.

Hata hivyo, akizungumza na gwiji la Brazil Ronaldo kwenye mtandao wa Twitch mwezi uliopita, nyota huyo alizungumzia pia mipango yake ya kustaafu.

"Nilikuwa nataniana na marafiki zangu kwamba nitastaafu nikiwa na umri wa miaka 32. Lakini ni utani tu. Kwa kweli, nitacheza hadi nitakapokuwa nimechoka kiakili," alisema.

Mahojiano hayo yanachochea fikra kwamba Neymar amekiwsha, ingawa ndo kwanza amefikisha miaka 30. Lakini pia unaongeza mafuta kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya Jumatano hii kati ya PSG na Real Madrid.

Neymar Jr na Vinicious J
Neymar Jr na Vinicious J

Vinicius mwenye umri wa miaka 21 amekuwa na kiwango bora msimu huu chini ya Carlo Ancelotti na kuwa moja ya vipaji vya soka vya kusisimua zaidi duniani.

Pengine hilo liliifanya Real kutumia euro milioni 45 kwa ajili ya kumsajili akiwa kinda mwenye umri wa miaka 16 mwaka 2017.

Na sasa ana nafasi ya kutimiza ndoto zake baada ya kuletwa Bernabeu katika kile kilichoonekana wakati huo kama jaribio la kumleta Neymar mwingine.

"Kati ya Vinicius na Neymar, kwa kiwango chake cha sasa, Vinicius ndiye anayejikuta katika nafasi nzuri ya kuamua mchezo huko Madrid," Paulo Vinicius Coelho, mmoja wa wachambuzi wa soka wa Brazil, aliiambia BBC.

"Haijulikani nini kitatokea baina yao katika kipindi hiki cha muda mfupi, lakini, kwa kile anachokifanya kila wiki, sina shaka kwamba Vinicius ni mshambuliaji mkubwa wa Brazil huko Ulaya hivi sasa. Neymar kawaida huanza msimu vizuri na kisha makali hupungua mwishoni. Anaweza kufanya kinyume msimu huu."

Ingawa Neymar hajafunga katika Ligi ya Mabingwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, ubora wake unabaki palrpale.

Kikwazo chake kikubwa alichonacho majeraha ambayo yamekuwa yakimrudisha nyuma pale PSG. Hadi sasa - kati ya mechi 255 ambazo PSG wamecheza tangu alipojiunga nao mwaka 2017, amecheza michezo 134 tu kati ya mechi 255.

Ni kitu ambacho kwa hakika hakisaidii kesi yake.

Hatumhitaji tena Neymar kwa sababu tunaye Vinicius'

Bila kujali Neymar anafanya nini, hawezi kuonekana kumfurahisha kila mtu. Ni kama uhusiano kati yake na mashabiki umefikia hatua ya mwisho ambapo hakuna kinachoweza kufanywa ili kuibadilisha.

"Kama Real Madrid itaichapa PSG, itaimarisha tu mtazamo kwamba hatumhitaji tena Neymar kwa sababu tuna Vinicius, lakini mambo hayako hivyo," Coelho alisema.

"Tunawahitaji wote wawili, kwa hivyo haturudii makosa yale yale tuliyofanya kwa kizazi kilichopita. Kwa sababu tofauti, Ronaldinho, Adriano na Kaka hawakujumuishwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2014 na tulienda huko na vijana wawili wenye umri wa miaka 22, Neymar na Oscar, wakiongoza mashambulizi yetu.

"Nchini Brazil, hatuna utamaduni wa kupita 'batni', Sio lazima iwe 'huu sio wakati wa Neymar tena, ni wakati Vinicius' sasa". Tunaweza kufanya vizuri tukiwa na wote Ulaya."

Bila kujali matokeo siku ya Jumatano, ni wakati wa Neymar kuonyesha uwezo wake kamili, hasa ukifikiria kwamba huu ni mwaka wa Kombe la Dunia.

Kwa upande wa Vinicius yeye bado ana safari ndefu mbele.

"Neymar bado hajafanikiwa kile, ambacho Wabrazili wengi, wanakiona kama kinapaswa kufanywa na wachezaji wetu, ambao ni kuwa mchezaji bora zaidi duniani na kushinda mataji makubwa," Bertozzi alihitimisha. "Ni jambo la kushangaza kwamba watu wengi walitarajia kutoka kwake na hajafanya hivyo hadi sasa.