Pigo baada ya kongamano la FIFA kuipiga marufuku ya Kenya kushiriki mashindano ya soka

Muhtasari

• Uthibitisho huo wa Alhamisi asubuhi uliona wanachama 198 wa Fifa wakipiga kura ya kusimamishwa kwa Kenya huku mmoja akipiga kura ya kupinga.

Harambee Stars
Image: FACEBOOK

Shirikisho la Soka la Kenya (FKF)  limepigwa marufuku kwa muda usiojulikana kutoshiriki shughuli zote za FIFA.

Hatua hii iliafikiwa katika mkutano wa Shirikisho la Fifa nchini Qatar Alhamisi asubuhi.

Uamuzi huo uliidhinishwa na wanachama 198 wa Fifa wakipiga kura ya kusimamishwa kwa Kenya huku mwanachama mmoja akipiga kura ya kupinga. 

Baraza la Fifa lilisimamisha FKF mnamo Februari 24, 2022 papo hapo kutokana na mshirika na watu wa tatu (serikali).

 Hii ilikuwa baada ya kutwaliwa kwa shughuli za FKF na ‘kamati ya uangalizi’ iliyoteuliwa na serikali badala ya kamati ya utendaji na katibu mkuu, ambayo ilihusisha ukiukaji mkubwa au Sheria za Fifa. 

Marufuku itaondolewa mara tu mahitaji muhimu yatakapotimizwa.

Mambo hayo ni pamoja na kurejeshwa kwa mamlaka ya kuendesha shughuli za soka kwa kamati ya utendaji na katibu mkuu