(Video) "Usiniulize ujinga!" Kocha wa Tusker FC afokea mwandishi wa habari baada ya kunyimwa ushindi dhidi ya Gor

Muhtasari

• Kocha wa Tusker FC, Robert Matano alighafilika baada ya refa kufutilia mbali bao dhidi ya Gor na kumaliza mchezo kwa sare.

• Mechi hiyo ilikumbwa na utata baada ya Tusker kufunga bao kunako dakika za mazidadi, bao lililokubaliwa lakini baadaye mashabiki wa Gor kuzua ikabidi refa alifutilie mbali.

Kocha wa Tusker FC, Robert Matano
Kocha wa Tusker FC, Robert Matano
Image: THE STAR

Wikendi iliyopita katika uwanja wa michezo wa manispaa ya Thika katika kaunti ya Kiambu, palishuhudiwa na kioja cha kustaajabisha wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Kenya baina ya Tusker na Gor Mahia.

Tukio hilo ambalo halikumfurahisha kocha wa timu ya Tusker, Robert Matano lilitokea kunako dakika za mazidadi ambapo timu zote zilikuwa sare ya nunge nunge na ghafla Tusker waakfunga bao ambao lilihalalishwa na refa.

Sekunde chache baadae mashabiki watundu wa timu ya Gor Mahia walianza kumfokea refa uwanjani huku wakianza kutupa mawe ambapo refa alilazimika kufanya uamuzi wa haraka baina ya kuliacha lile goli lisimame na apigwe mawe hadi kufa au alifutilie mbali bao na kuokoa uhai wake.

Refa alichukua uamuzi wa kuokoa maisha yake kwa kulifutilia mbali lile bao la Tusker na hapo hapo kuumaliza mchezo.

Tukio hilo lilimghadhabisha kocha Matano wa Tusker ambapo baada ya mechi alizushiana na waandishi wa habari waliotaka kujua maoni yake kuhusu matoke ya mechi ambayo kulingana na yeye alinyimwa ushindi wa wazi tena mchana peupe.

“Kocha, na matokeo haya, ni vizuri kusema kwamba ligi imeenda?” aliuliza mwandishi wa habari.

“Sijui. Sijui usiniulize upuzi pia?” alijibu kocha Matano kwa ghadhabu kali.

 

Video: Michael Were Mukhusia