(VIDEO) Shabiki akimbia uchi uwanjani baada ya timu yake kushinda

Muhtasari

• Shabiki huyo alijawa na furaha baada ya timu yake Ahsante Kotoko kuifunga Accra Heats of Oak bao moja kwa nunge Jumapili iliyopita.

Shabiki wa Asante Kotoko akimbia uchi
Shabiki wa Asante Kotoko akimbia uchi
Image: Sika Fotos//Joseph Boateng

Jumapili iliyopita palishuhudiwa kioja cha kupofusha macho nchini Ghana wakati shabiki mmoja wa mpira wa miguu kuvuka mipaka ya kusherehekea mchezo huo ambapo alivua nguo zote na kubaki na suti ya Mungu huku akikimbia uwanja mzima mithili ya punda aliyeumwa na mbung’o.

Shabiki huyo wa timu ya Asante Kotoko aliongezea ladha ya aina yake katika macho ya mashabiki waliokuwa wamefurika ugani Baba Yara mjini Kumasi, Nigeria kushuhudia mtangange mkali baina ya Ahsante Kotoko na Accra Heats of Oak.

Timu ya Asante Kotoko ilishinda mchezo huo bao moja kwa nunge, bao lililotokana na mkwaju wa penati na kutokana na ugumu wa mechi ulivyokuwa, pindi tu baada ya kipenga cha mwisho mashabiki wa Kotoko walishangilia kwa furaha lakini huyu mmoja akawa mwenye furaha ya kipekee.

Kwake, nguo hazikuwa na umuhimu wowote tena zaidi ya beramu ya timu yake ambayo aliipeperusha kwa madoido huku akikimbia uwanja mzima, na nyuma yake walinzi wa uwanjani walimfuata unyo ja umbwa na sungura kumkamata ili kumzuia. Tatizo mtu ukiwa umevalia suti ya Mungu kushikika ni mbinde aisee!