logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sean Dyche atimuliwa Burnley

Mkufunzi wa Burrnley Sean Dyche amefutwa kazi huku ikiwa zimesalia mechi 18 ligi itamatike.

image
na Davis Ojiambo

Michezo15 April 2022 - 02:14

Muhtasari


  • • Klabu ya Burnley imemfukuza kazi Meneja wao Sean Dyche ikiwa zimebakia mechi nane tu kumaliza msimu huu kwenye Ligi ya England.
  • • Meneja Msaidizi Ian Woan, kocha Steve Stone na kocha wa makipa Billy Mercer nao wameondoka.
Sean Dyche

Klabu ya Burnley imemfukuza kazi Meneja wao Sean Dyche ikiwa zimebakia mechi nane tu kumaliza msimu huu kwenye Ligi ya England.

Burnley ambao wamepoteza mara 5 kati ya mechi 6 zilizopita kwa sasa wanashika nafasi ya 18.

Dyche alikuwa Meneja wa Ligi ya England aliyekaa kwa muda mrefu zaidi , akiwa amejiunga na klabu hiyo  mnamo Oktoba 2012.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Alan Pace amenukuliwa akisema kuwa, “ ilikuwa ni uamuzi mgumu sana kuamua kuachana na Dyche lakini tunahisi kuwa mabadiliko yanahitajika.”

Meneja Msaidizi Ian Woan, kocha Steve Stone na kocha wa makipa Billy Mercer nao wameondoka.

Kwa sasa Burnley wanashikilia mafasi ya 18 kwenye jedwali la ligi kuu nchini Uingerezawakiwa na alama 24 baada ya kushiriki mechi 30.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved