Sean Dyche atimuliwa Burnley

Muhtasari

• Klabu ya Burnley imemfukuza kazi Meneja wao Sean Dyche ikiwa zimebakia mechi nane tu kumaliza msimu huu kwenye Ligi ya England.

• Meneja Msaidizi Ian Woan, kocha Steve Stone na kocha wa makipa Billy Mercer nao wameondoka.

Sean Dyche
Sean Dyche
Image: Instagram

Klabu ya Burnley imemfukuza kazi Meneja wao Sean Dyche ikiwa zimebakia mechi nane tu kumaliza msimu huu kwenye Ligi ya England.

Burnley ambao wamepoteza mara 5 kati ya mechi 6 zilizopita kwa sasa wanashika nafasi ya 18.

Dyche alikuwa Meneja wa Ligi ya England aliyekaa kwa muda mrefu zaidi , akiwa amejiunga na klabu hiyo  mnamo Oktoba 2012.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Alan Pace amenukuliwa akisema kuwa, “ ilikuwa ni uamuzi mgumu sana kuamua kuachana na Dyche lakini tunahisi kuwa mabadiliko yanahitajika.”

Meneja Msaidizi Ian Woan, kocha Steve Stone na kocha wa makipa Billy Mercer nao wameondoka.

Kwa sasa Burnley wanashikilia mafasi ya 18 kwenye jedwali la ligi kuu nchini Uingerezawakiwa na alama 24 baada ya kushiriki mechi 30.