Cristiano Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez wametangaza kifo cha mtoto wao wa kiume

Muhtasari

• Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 na Rodriguez mwenye umri wa miaka 28 walikuwa wakitarajia kujifungua pacha.

• Timu ya Man United ilichapisha ujumbe katika mtandao wao wa twitter: Uchungu wako ni uchungu wetu.

• Mtoto wao wa kike alinusurika , na wanasema kuzaliwa kwake kuliwapatia nguvu kuishi muda huu wakiwa na matumiani na furaha.

Ronaldo na Mkewe katika hafla ya siku yake ya kuzaliwa
Image: Christiano Ronaldo (Facebook)

Nyota wa timu ya Manchester United Cristiano Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez wametangaza kifo cha mtoto wao wa kiume , wakisema kwamba ni uchungu mkubwa mbao mzazi yeyote anaweza kuhisi.

Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 37 na Rodriguez mwenye umri wa miaka 28 walikuwa wakitarajia kujifungua pacha.

Mtoto wao wa kike alinusurika , na wanasema kuzaliwa kwake kuliwapatia nguvu kuishi muda huu wakiwa na matumiani na furaha. ''Mwana wetu wa kiume wewe ni malaika wetu. Tutakupenda maisha yetu yote'', waliandika

Katika taarifa iliochapishwa katika mtandao wa kijamii, walisema : Ni huzuni kubwa kwamba tunatangaza kifo cha mtoto wa kiume aliyefariki. ''Tumeghdhabishwa na kifo hiki na sasa tunaomba kuwa na faragha wakati huu mgumu''.

Wawili hao walitangaza kupata ujauzito huo mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Timu ya Man United ilichapisha ujumbe katika mtandao wao wa twitter: Uchungu wako ni uchungu wetu. ''Tunakutumia risala za mapenzi na nguvu kwa wewe na familia yako wakati huu''

Mchezaji mwenza Marcus Rashford aliandika: "Fikra zetu ziko nawe na ndugu yake Georgina , pole sana.."

Timu ya zamani ya Ronaldo, Real Madrid rais wake pamoja na bodi ya wakurugenzi walisema "wamehuzunishwa sana" na kuongeza: "Real inahisi maumivu ya wazazi hao na inawatakia subra na nguvu wakati huu".

Klabu za Manchester City, Leeds United na ligi ya Premia pia wametuma ujumbe katika twitter wakituma salamu za rambirambi.

Ronaldo ana mtoto kwa jina Cristiano Jr, ambaye alizaliwa 2010 pamoja na pacha Eva na Mateo ambao walizaliwa 2017. Pia ana mtoto wa kike kwa jina Rodriguez -Alana Martina aliyezaliwa 2017.