Erik ten Hag: Man Utd wanaweza kutarajia nini kutoka kwa meneja wao mpya?

Muhtasari

•Anatoka mashariki mwa Uholanzi ambapo watu wa sehemu hizo ni wanyenyekevu mno na wengi huwa na lahaja.

Erik ten Hag
Erik ten Hag
Image: EURO SPORT

Erik ten Hag hakuwahi kuwa mmoja wa watu ambao waliweka wazi kuwa alikuwa na matamanio makubwa ya kuwa mmoja wa makocha wakuu duniani. Ni mtu mnyenyekevu sana

Hilo ni kutokana na maeneo anayotoka. Anatoka mashariki mwa Uholanzi ambapo watu wa sehemu hizo ni wanyenyekevu mno na wengi huwa na lahaja.

Lakini licha ya kutoka katika sehemu hiyo, hali ya Ten Tag ni tofauti . Kifedha - hana mshawasha wa kukimbilia kazi kubwa katika awamu yoyote ya maisha yake kwasababu anatoka katika familia tajiri sana ambapo baba na ndugu zake ni mamilionea. Wanamiliki kampuni ya majumba na kampuni nyengine za fedha.

Babake alimtaka aende kusimamia kampuni hiyo lakini tangu akiwa na umri mdogo Erik alikuwa mchezaji mzuri wa kandanda - alikuwa nyota wa klabu ya FC Twente akiwa beki - hivyobasi ilikuwa wazi kwamba hangekuwa tayari kufanya kazi kama hiyo.

Utajiri wa familia yake una maana kwamba ahitaji kazi kubwa.. Anafahamu kwamba ahitaji soka ili kuishi, hivyobasi anaweza kufuata anachotaka kufanya, ambapo wakufunzi wengine wangetumia kila njia kusalia katika kazi hiyo.

Filosofia yake imekuwa kuwa kama ile ya Pep Guradiola na Johan Cruyff. Anapenda kushambulia na kutengeneza fursa uwanjani.

Niliifuatalia klabu ya PSV Eindhoven kwa muda wakati alipokuwa naibu mkufunzi, muda huohuo ambapo alikuwa naibu wa mkufunzi Steve McClaren katika klabu ya FC Twente.

Alikuwa maarufu . hakujaribu kuingia kwa lazima lakini wakufunzi walimtegemea sana , walifurahia sana kushirikiana naye.

Wakati alipokuwa katika klabu ya Bayern kama kocha wa timu ya ziada alipenda kazi yake sana. Ilikuwa ni kama ametimiza ndoto yake kufanya kazi na mkufunzi Pep Guradiola ambaye alikuwa akifanya jinsi anvyopenda kufanya kazi.

Aliniambia kwamba alipenda sana kutumia muda wake mwingi na Guardiola, alipenda kuzungumza naye. Alilazimika kuipatia timu kikosi cha kwanza .

Haitakuwa rahisi kwa wachezaji kushirikiana naye kwasababu yeye kama Guardiola, ni mtu anayependa soka sana.

Ili kupata mbinu ya kucheza kama ilivyo Ajax , inahitaji kazi nyingi na idadi kubwa ya washambuliaji.

Mbinu hiyo inawacha mianya mikubwa hivyobasi walinzi wa timu watahitajika kupanda juu zaidi ili kuziba mapengo yaliowachwa . Ni mfumo unaohitaji kujitolea na hatari sana hivyobasi wachezaji ni sharti wajue kwamba pasi wanayotoa itamfikia mchezaji anayelengwa na kwamba hakutakuwa na makosa.

Lakini ukufunzi wa mtu huyu ni mzuri na kwamba wachezaji wake husema wamejifunza mengi kutoka kwake.

Huku makocha wengi wakilenga kikosi cha kwanza, Ten Hag hutumia muda wake mwingi katika mafunzo uwanjani. Katika klabu ya Manchester united hatowategemea wachezaji nyota kama vile Ronaldo au Maguire, atampatia sikio mchezaji wa 19 au 20. Ameshirikiana na wachezaji wenye tabia tofauti na hajali ni saa ngapi ameshirikiana nao, atawaptia muda wake wote.

Hivyo ndio sababu yeye hupewa heshima na wachezaji kwasababu wanaona juhudi anazoweka katika kuimarisha mchezo wao binafsi.

Hata wale wanaotoka katika mazingira magumu - ambao wanaoonekana kuwa mizigo katika timu zao pengine - iwapo anaona kwamba talanta ipo atahakikisha kwamba wanashirikishwa.

Haogopi kuchukua kazi ya klabu ya Manchester United. Lakini atapendelea kuwa katika gwanda la mazoezi kwa saa nyingi. Hajitambui kuwa mtu anayetakiwa kufanya kazi katika ofisi -kama ingekuwa hivyo angejiunga na kampuni ya babake.

Hapendelei kuwa katika simu kila mara akizungumza na maajenti. Ni kutokana na hali ndio atahitaji mkurugenzi wa michezo au msaidizi mwenye uwezo kama huo .

Kwangu mimi , itakuwa makosa kwa yeye kufikiria kwamba kati ya majukumu yake ni kuingiana na ukufunzi wa makocha Uingereza.

Hangetaka kuingia katika klabu hiyo akifikiria ataimiliki klabu yote ya Manchester United. Atapendelea kuifanya klabu hiyo itambuliwe tena - na ataboresha hilo kwa kuvalia jezi ya mafunzo.

Suala jingine ni kwamba Ten Hag hajawahi pendelea kusimama mbele ya kamera. Hilo litakuwa changamoto kwake na huenda akapata shida kuwasilisha ujumbe wake.

Iwapo angeenda kujiunga na klabu ya Ujerumani , asingekuwa na tatizo kama hilo kwasababu anapoishi ni mpakani na Ujerumani.

Kila mtu katika eneo hilo anazungumza Kijerumani kama lugha yake ya pili.