Kurt Zouma: Beki wa West Ham akiri kosa la kumpiga paka wake

Muhtasari
  • Kaka yake Zouma Yoan, anayechezea Dagenham na Redbridge, alikiri kosa moja baada ya uchunguzi wa RSPCA
Kurt Zouma

Beki wa West Ham United Kurt Zouma amekiri kosa la kumpiga teke na kumpiga paka wake kwenye video ambayo pia ilimuonesha akisema "Naapa nitamuua".

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikiri makosa mawili chini ya Sheria ya Ustawi wa Wanyama katika katika Mahakama ya Thames.

Kaka yake Zouma Yoan, anayechezea Dagenham na Redbridge, alikiri kosa moja baada ya uchunguzi wa RSPCA. Yoan, 24, alirekodi tukio hilo, ambalo lilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kesi imeahirishwa hadi Juni 1. Anwani za ndugu hao zilizuiwa kufuatia agizo la mahakama.

Mahakama ilielezwa kuhusu picha za video za kutatanisha za tukio hilo, ambazo zilinakiliwa nyumbani kwa mchezaji huyo wa West Ham na kuchapishwa kwenye Snapchat na emoji za 'kucheka' na kaka yake tarehe 6 Februari.

Zouma alionekana akimzungusha paka huyo, kabla ya kumrushia jozi ya viatu na kumpiga kichwani.