'Mauzo ya Chelsea 'bado yana vikwazo vikubwa kuvishinda'

Muhtasari

•Chelsea wamekubaliana kuhusu mkataba unaofadhiliwa na mashirika ya kibinafsi unaoongozwa na mwekezaji wa Marekani Todd Boehly

•Inafahamika kwamba, kwa sababu mmiliki Roman Abramovich ana pasipoti ya Ureno, uuzwaji huo unahitaji kupewa leseni na mamlaka katika nchi hiyo pia.

Mmiliki wa Chelsea Roma Abrahamovich
Mmiliki wa Chelsea Roma Abrahamovich
Image: BBC

Serikali ya Uingereza iko tayari kuidhinisha mauzo ya Chelsea ya £4.25bn ndani ya saa 24 zijazo, BBC Sport imebaini.

Hata hivyo, mpango huo "bado una vikwazo vikubwa vya kuvishinda" kwa mujibu wa chanzo cha ndani cha Whitehall.

Inafahamika kwamba, kwa sababu mmiliki Roman Abramovich ana pasipoti ya Ureno, uuzwaji huo unahitaji kupewa leseni na mamlaka katika nchi hiyo pia.

Mawaziri sasa wanasemekana kuwa katika "majadiliano makali" na wenzao katika Tume ya Ulaya ili kuwahakikishia wanaohitaji kuidhinisha mpango huo.

Chelsea wamekubaliana kuhusu mkataba unaofadhiliwa na mashirika ya kibinafsi unaoongozwa na mwekezaji wa Marekani Todd Boehly, mmiliki mwenza wa timu ya besiboli ya LA Dodgers.

Klabu hiyo iliuzwa kabla ya mmiliki Abramovich kuwekewa vikwazo kwa madai ya kuwa na uhusiano na rais wa Urusi Vladimir Putin kufuatia uvamizi wa Ukraine.

Kisha serikali ilitoa leseni maalum kwa Chelsea kuendelea kufanya kazi, ambayo itaisha tarehe 31 Mei.

Wiki iliyopita BBC iligundua kuwa serikali ilikuwa na wasiwasi kwamba mpango huo unaweza kuwa katika hatari ya "kusambaratika" kutokana na kukosekana kwa maelewano na klabu kuhusu mapato ya mauzo yoyote.

"Kila mtu anataka kufanikisha mpango huo, lakini kutokana na hali ngumu ya mkataba na muundo wa umiliki wa Chelsea, hakuna kitu rahisi," kilisema chanzo cha Whitehall.

"Muda unaenda kwa kasi, mpango huu lazima ukamilike mwishoni mwa Jumanne, vinginevyo klabu itakuwa hatarini."