Uingereza yaidhinisha ombi la kampuni ya Todd Boehly kununua Chelsea

Muhtasari

•Chelsea iliuzwa mwezi Machi kabla ya mmiliki Roman Abramovich kuwekewa vikwazo kutokana na uhusiano wake na rais wa Urusi Vladimir Putin.

•Serikali haitaki Abramovich kupokea mapato yoyote kutokana na mauzo hayo na badala yake yawekwe kwenye akaunti ya benki iliyofungiwa ili kuchangwa kwa mashirika ya misaada.

Todd Boehly ataongoza kundi litakalomilliki Chelsea
Todd Boehly ataongoza kundi litakalomilliki Chelsea
Image: BBC

Serikali ya Uingereza imeidhinisha ombi la muungano wa makampuni ya kibiashara unaoongozwa na mmiliki mwenza wa LA Dodgers Todd Boehly la kutaka kununua klabu ya soka ya Chelsea kwa kima cha pauni bilioni 4.25.

Klabu hiyo ya London iliuzwa mwezi Machi kabla ya mmiliki Roman Abramovich kuwekewa vikwazo kutokana na uhusiano wake na rais wa Urusi Vladimir Putin.

Siku ya Jumanne, Ligi Kuu ilisema muungano huo ulipitisha mtihani wa wamiliki na wakurugenzi. Chelsea imekuwa ikifanya kazi chini ya leseni maalum ya serikali ambayo muda wake unaisha tarehe 31 Mei.

"Jana usiku serikali ya Uingereza ilifikia hatua ambapo tunaweza kutoa leseni inayoruhusu uuzaji wa Chelsea," msemaji wa serikali alisema katika taarifa yake Jumatano.

Chelsea imekuwa ikihudumu kwa leseni maalum ya serikali ambayo muda wake unamalizika Mei 31.

Serikali haitaki Abramovich kupokea mapato yoyote kutokana na mauzo hayo, ambayo badala yake yataingia kwenye akaunti ya benki iliyofungiwa ili kuchangwa kwa mashirika ya misaada.

Taarifa hiyo iliongeza: "Kufuatia adhabu ya Roman Abramovich, serikali imefanya kazi kubwa kuhakikisha Chelsea imeweza kuendelea kucheza soka.

Lakini siku zote tumekuwa tukiweka wazi kwamba mustakabali wa muda mrefu wa klabu unaweza kupatikana tu chini ya mmiliki mpya.

"Kufuatia kazi kubwa, sasa tumeridhika kwamba mapato kamili ya mauzo hayatamnufaisha Roman Abramovich au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa. Sasa tutaanza mchakato wa kuhakikisha mapato ya mauzo yanatumika kwa sababu za kibinadamu nchini Ukraine, kusaidia wahasiriwa wa vita