Eto'o akiri kukwepa kodi akiwa Barcelona

Muhtasari

•Mahakama katika jiji hilo imempa kifungo cha miezi 22 jela na faini - lakini ataepuka kwenda jela kwa sababu alikiri hatia.

Image: HISANI

Nyota wa kandanda wa Cameroon Samuel Eto'o amekiri kufanya ulaghai wa mamilioni ya dola kwenye ulipaji wa kodi yake wakati alipokuwa akiichezea Klabu kubwa ya Uhispania Barcelona.

Mahakama katika jiji hilo imempa kifungo cha miezi 22 jela na faini - lakini ataepuka kwenda jela kwa sababu alikiri hatia.

Kwa ujumla, Eto'o atalazimika kulipa zaidi ya $8m (£6.5).

Uamuzi wa mahakama ulisema Eto'o na wakala wake walikwepa kwa makusudi ushuru wa mapato ulitokana na hatimiliki ya picha kati ya 2006 na 2009.

Wakati wa enzi zake za uchezaji, Eto'o alionekana kuwa mmoja wa washambuliaji bora duniani. Sasa ni rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon.