Wafcon: Michuano ya Kombe la Afrika miongoni mwa wanawake yarudi

Wachezaji wa Nigeria
Wachezaji wa Nigeria
Image: BBC

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika miongoni mwa Wanawake (WAFCON) inarejea mwezi huu baada ya kukosekana kwa miaka minne, huku mashindano makubwa zaidi ya wanawake barani humo yakipanuka na kushirikisha timu 12.

Baada ya kuonyesha vipaji vya hali ya juu kutoka kwa Mnigeria Mercy Akide-Udoh katika miaka ya 1990 hadi fowadi wa Afrika Kusini Thembi Kgatlana mara ya mwisho, mashindano ya mwaka huu pia yataamua mechi nne za Afrika za kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake 2023.

Itaandaliwa katika ardhi ya Afrika Kaskazini kwa mara ya kwanza na Morocco, huku michezo ikichezwa katika viwanja vitatu vya Rabat na Casablanca kuanzia Julai 2-23.

Nigeria ilinyanyua kombe hilo katika matoleo matatu yaliyopita na wameshinda mara tisa katika WAFCON 11 zilizopita, na timu hiyo iliyoorodheshwa juu zaidi barani bado ndiyo timu itakayotoa ushindani mkali katika kinyang’anyiro hicho

Cameroon na Afrika Kusini ni miongoni mwa wapinzani wao wa karibu, lakini kutokana na nchi nne kushiriki kwa mara ya kwanza huenda mambo yasiwe rahisi