Leonel Messi yuko mbioni kuvunja rekodi ya Dani Alves

Messi kwa sasa amepata mataji 41 katika maisha yake ya soka

Muhtasari

•Maxwell na Andres Iniesta wanashika nafasi ya nne kwa kupata mataji mengi.

•Tangu ajiunge na Paris Saint Germain 2021, Lionel Messi ameongeza mataji mawili kwenye  - Ligue 1 (2021-22) na Trophee des Champions (2022).

Messi apokea tuzo la mchezaji bora kwa mara ya 7
Messi apokea tuzo la mchezaji bora kwa mara ya 7
Image: BALLON D'OR TWITTER

Leonel Messi sasa yuko mbioni kukuwa na mataji sawa na Dani Alves ambaye ni mchezaji mwenye taji nyingi sana duniani. 

Messi kwa sasa amepata mataji 41 katika maisha yake ya soka, ikibakia tu taji moja  kumfikia Dani Alves.

Messi alishinda mataji 35 akiwa Barcelona (2004-2021) huku akishinda mataji manne za kimataifa, likiwemo la Copa America 2021. Muargentina huyo pia alishinda medali ya dhahabu ya Olimpiki huko Beijing 2008.

Tangu ajiunge na Paris Saint Germain 2021, Lionel Messi ameongeza mataji mawili kwenye  - Ligue 1 (2021-22) na Trophee des Champions (2022).

Dani Alves beki huyo wa Brazil alishinda tuzo yake ya kwanza ya kitaalamu akiwa na klabu ya nyumbani ya Bahia.

Baada ya kushinda mataji matano ndani ya miaka sita akiwa na Sevilla,Beki huyo  alihamia Barcelona kwa pauni milioni 23 na akaendelea kushinda mataji 23 - ikiwa ni pamoja na mataji sita ya La Liga na matatu ya UEFA Champions League.

Baada ya muda mrefu wa kubeba taji akiwa Juventus (2016-17 - mataji mawili), Paris Saint-Germain (2017-19 - mataji sita) na Sao Paulo (2019-21 - kombe moja), Alves ajiunga na timu ya Mexico ya UNAM mnamo 2022 baada ya kumalizika kwa kipindi chake cha pili akiwa Barcelona.

Maxwell na Andres Iniesta wanashika nafasi ya nne kwa kupata mataji mengi.

Wawili hao, ambao waliwahi kuwa wachezaji wenza katika klabu ya Barcelona, ​​wana mataji 37 kila mmoja.