Koulibaly Kalidou apata kibali kutoka kwa John Terry kuvalia Jezi nambari 26

Wanablues wanatarajiwa kuanza msimu mpya kwa mechi ya London derby dhidi ya Tottenham

Muhtasari

•Nahodha wa Senegal Kalidou Koulibaly alilazimika kutafuta baraka za beki wa zamani wa Chelsea John Terry ili kuvaa jezi yake yenye namba 26.

•Kalidou Koulibaly alijiunga na wababe hao wa Uingereza baada ya kuaga  klabu ya Napoli ya Italia.

Kalidou Koulibaly na John Terry
Kalidou Koulibaly na John Terry
Image: UGC

Hatimaye Kalidou Koulibaly ameruhusiwa kuvaa jezi nambari 26 akiwa Chelsea na nahodha wa zamani John Terry.

Beki huyo wa kati wa Senegal alijiunga na wababe hao wa Uingereza baada ya kuaga  klabu ya Napoli ya Italia.

Kupitia kwa mazungumzo yao kwa njia ya simu, iliyonaswa kwenye video, Koulibaly alilazimika kutafuta baraka za John Terry kuvaa shati nambari 26 iliyovaliwa na mlinzi huyo maarufu wa Uingereza.

"John nilitaka kukuuliza kitu kwa sababu kama unavyojua nilivalia jezi nambari 26 huko Napoli, na tangu uondoke kwenye klabu ya Chelsea hakuna mtu aliyechukua  jezi nambari 26, sijui kwa nini mtu hataki kuichukua, nilitaka kukuuliza ikiwa inawezekana niichukue,” Koulibaly aliuliza kupitia simu.

John Terry alijibu: "Kusema kweli jezi nambari 26 ilikuwa wa kipekee sana kwangu, hakuna shida mwenzangu, ninakushukuru sana kwa kupiga simu na sio shida kuipokea, naifurahia sana wazo lako"

Nambari anayoipenda zaidi Koulibaly ni 26, na amekuwa akiitumia kwenye jezi yake wakati akiwa Napoli Italia.

John Terry aliifanya namba hiyo kuwa maarufu nchini Uingereza kufuatia huduma zake bora akiwa katika klabu ya Chelsea.

Chelsea wanajiandaa kwa ajili ya kuanza kwa msimu mpya, huku wakianza mapambano kali dhidi ya Tottenham Hotspurs ya Antonio Conte.

Koulibaly anatarajiwa kuanza pamoja na mlinzi  Thiago Silva kwenye   safu ya ulinzi Jumapili, Agosti 14, 2022