Benni McCarthy ateuliwa mkufunzi wa kikosi cha kwanza cha Manchester United

Sasa amekubali jukumu na United kuanza kazi ya ukocha huko Uropa.

Muhtasari

• Benni McCarthy anatambulika sana kama mmoja wa washambuliaji  bora barani ulaya enzi zake.

Wakufunzi wa Manchester United
Wakufunzi wa Manchester United
Image: Handout

Klabu ya Manchester United imemteua Benni McCarthy kama kocha wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Klabu hicho kimefanya nyongeza mpya kwenye safu yake ya ukocha chini ya Erik Ten Hag.

Erik Ten Hag alisema kuwa kuongezwa kwa McCarthy katika safu ya ukufunzi, kutawezesha klabu hicho kusajili matokeo mazuri na kupigania mataji makuu. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 44 atafanya kazi kwa ukaribu na kikosi cha kwanza huko Carrington na atatoa mafunzo maalum kwa washambuliaji.

Benni McCarthy anatambulika sana kama mmoja wa washambuliaji  bora barani ulaya enzi zake.

Kutokana na tajiriba yake  ya hali ya juu ya ushambulizi, McCarthy hatashughulikia tu  wachezaji washambulizi  bali atazingatia pia uboreshaji wa wachezaji wengine kwa ujumla.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Afrika Kusini amekuwa meneja wa timu kama Cape Town City na Amazulu tangu 2017, lakini aliacha jukumu lake na wachezaji hao mwezi Machi baada ya kuwaongoza katika Ligi ya Mabingwa ya CAF.

Sasa amekubali jukumu na United .

McCarthy ni shabiki wa United na uzoefu katika Ligi kuu ya Uingereza, alikaa misimu minne na  Klabu ya Blackburn Rovers na miwili katika klabu ya West Ham United.