Mwanamke aeleza mahakama jinsi Benjamin Mendy alivyojaribu'kumshawishi' kufanya ngono naye

Mwanamke huyo alidai kuwa alibakwa na beki huyo wa zamani wa Manchester City kwa takriban "sekunde 20"

Benjamin Mendy, 28, anakanusha makosa manane ya ubakaji, shtaka moja la kujaribu kubaka na moja la unyanyasaji wa kingono.
Benjamin Mendy, 28, anakanusha makosa manane ya ubakaji, shtaka moja la kujaribu kubaka na moja la unyanyasaji wa kingono.
Image: BBC

Mwanasoka Benjamin Mendy anadaiwa kuwa alijaribu kumshawishi mwanamke ili kufanya nae ngono baada ya kumtoa mwanamke huyo kwenye mkusanyiko wa watu na kumpeleka sehemu nyingine ya peke yao ndani ya jumba hilo la kifahari.

Katika mahojiano ya polisi yaliyooneshwa katika Mahakama ya Chester Crown, mwanamke huyo alidai kuwa alibakwa na kijana huyo wa miaka 28 kwa takriban "sekunde 20" Julai 2021.

Alisema upinzani wake kukataa kufanya kitendo haukuwa kikwazo kwa mchezaji wa Manchester City na ilikuwa "kama kubishana na ukuta wa matofali".

Mendy anakanusha mashtaka nane ya ubakaji, jaribio la ubakaji na unyanyasaji wa kingono. Mwanamke huyo alidai kuwa alimpeleka katika chumba cha sinema nyumbani kwake huko Mottram St Andrew, Cheshire.

Alisema alikuwa amealikwa ambapo watu walikuwa wakinywa pombe na kucheza michezo mbalimbali. Alisema: "Nilikuwa kama, 'Sitaki kufanya chochote, sikujui wewe'.

Mwanamke huyo alieleza mahakama kwamba hakuwafahamu wageni wengine kwenye hafla hiyo vizuri na alihisi asingeweza kuondoka tu.