(+video) Umtiti atokwa na machozi baada ya kutambulishwa Lecce kutoka Barcelona

Umtiti alijiunga na Barcelona akitokea Lyon mwaka 2018.

Muhtasari

• Beki huyo matata alikuwa katika kikosi cha Ufaransa kilichoshinda kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

• Alijiunga na Lecce kwa mkopo baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Xavi kutokana na majeraha ya muda kwa muda.

Beki wa kimataifa wa Ufaransa ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiisakatia Barcelona ya Uhispania Samuel Umtiti juzi alitangazwa kuhamia timu ya Lecce ya Uitaliano kwa mkopo baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Xavi wa Barcelona.

Umtiti mwenye umri wa miaka 28 alikosa nafasi katika kikosi cha kwanza kutongana na majeraha ambayo yamekuwa yakimuandama kwa muda.

Baada ya uhamisho wake wa mkopo Kwenda Lecce, katika hafla ya utambulisho wake kwa mashabiki, Umtiti alishindwa kujiuzia kabisa na kudondokwa na machozi huku akishindwa hata kuongea kutokana na kulemewa na hisia za jinsi mashabiki walikuwa wanaliimba jina lake kwa vifijo na furaha kubwa mpaka kujihisi kigogo mweney uswadi wa mfalme.

Katika video hiyo ambayo imesambazwa kweney mtandao wa Twitter, Umtiti anaonekana akizingirwa na wanahabari wengi wakimtaka kusema japo neno moja ila shangilio kutoka kwa mshabiki kulizua hisia ndani mwake na hisia hizo kwa mwanaume mwenye mapande yake sita zilidhihirika kupitia machozi.

Umtiti alijiunga na Barcelona mwaka 2018 akitokea Lyon ya Ufaransa na alikuwa mmoja kati ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichoshinda kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi.

Uhamisho wa mkopo wa Umtiti ni ushindi kwa pande zote mbili; Barca na Leece kwani miamba hao wa Catalan hatimaye wataweza kumsajili Jules Kounde, huku Leece wakipata beki wa juu bila kulazimika kugharamia mishahara yake, kulingana na jarida la Goal.com