Dili zilizokamilika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho wa wachezaji

Baadhi ya wachezaji walisajiliwa kutoka ligi hiyohiyo ya Uingereza huku wengine wakichukuliwa kwingine.

Muhtasari

•Siku ya mwisho ya soko la uhamisho wa wachezaji katika EPL lilikuwa na shughuli nyingi huku wachezaji mbalimbali wakihama kutoka vilabu vyao na kujiunga na vilabu vipya aidha kwa mkopo au uhamisho wa kudumu.

Aubameyang, Arthur Melo, Hector Bellerin, Martin Dubvraka
Image: HISANI

Dirisha ya uhamisho katika ligi kuu ya Uingereza ilifungwa usiku wa Septemba 1, 2022 baada ya kuwa wazi kwa takriban miezi mitatu.

Siku ya mwisho ya soko la uhamisho wa wachezaji katika EPL lilikuwa na shughuli nyingi huku wachezaji mbalimbali wakihama kutoka vilabu vyao na kujiunga na vilabu vipya aidha kwa mkopo au uhamisho wa kudumu.

Baadhi ya wachezaji walisajiliwa kutoka ligi hiyohiyo ya Uingereza huku wengine wakichukuliwa kutoka kwa mataifa mengine.

Hii hapa orodha ya uhamisho ambao ulikamilika kabla ya Septemba 1, 11.59PM, masaa ya Uingereza:

1. Pierre Emerick Aubameyang: Barcelona- Chelsea (£10.3m)

2. Marcos Alonso: Chelsea- Barcelona (Uhamisho wa bure)

3.Dennis Zakaria: Juventus- Chelsea (Mkopo)

4. Hector Bellerin: Arsenal-Barcelona (Uhamisho wa bure)

5. Ainsley Maintland-Niles: Arsenal-Southampton (Mkopo)

6. James Garner: Manchester United-Everton (£15 m)

7. Martin Dubravka: Newcastle- Manchester United (Mkopo)

8.Antony Matheus dos Santos -Ajax- Manchester United (£85m )

9. Arthur Melo: Juventus-Liverpool (Mkopo)

10. Manuel Akanji: Borrusia Dortmund- Manchester City (£15.1m)

11. Jan Bednarek: Southampton- Aston Villa (Mkopo)

12. Leander Dendoncker: Wolves- Aston Villa (Ada isiyojulikana)

13. Duje Caleta: Olympique Marseille- Southampton (£8)

14. Juan Larios:Manchester City- Southampton (£6m)

15.Yan Valery: Southampton-Angers (Ada isiyojulikana)

16. Andre Gomes: Everton- Lille (Mkopo)

17. Carlos Vinicius: Benfica-Fulham (£4m)

18. Daniel James; Leeds-Fulham (Mkopo)

19. Billy Gilmour: Chelsea-Brighton (£9m)

20. Willian: Corithians-Fulham  (Ada isiyojulikana).