Wachumba Wachina wasema Fabregas aliwafanya kupendana, wamtaka aibariki ndoa yao

Wewe ndio sababu nilianza kutazama mpira wa miguu

Muhtasari

• Bado nakumbuka nyakati za usiku za shule yangu ya upili nilikuwa nikisikiliza redio moja kwa moja ya Arsenal

Anorld Wang Yuaren na mpenzi wake
Anorld Wang Yuaren na mpenzi wake
Image: Twitter//Anorld Wang Yuaren

Cesc Fabregas ni kiungo wa kati wa Uhispania aliyeshabikiwa na wengi enzi zake akisakatia klabu ya Arsenal, Barcelona na Chelsea miongoni mwa timu kubwa katika soka la Uropa.

Fabregas alishabikiwa na wengi kutokana na weledi wake wa kuchanja pasi nyerezi zilizounganisha mabao katika timu nyingi alizozichezea.

Lakini pia wengi walimjua zaidi kipindi anachezea Arsenal katika ujana wake.

Wakati Fabregas anashughulika kutoa pasi nyingi awezavyo ndani ya Arsenal, hakuwahi jua kwamba kuna watu wengi waliokuwa wakipata himizo kutoka kwake. Himizo ambalo liliunganiisha baadhi kupendana kutokana na kupenda mchezo wake.

Hili lilidhihirika wazi baada ya shabiki wa muda mrefu wa Cesc Fabregas kutoka Uchina, Arnold Wang Yuaren kujieleza kweney ujumbe mrefu Twitter kwamba alipata mchumba wake kutokana na kupenda kumshabikia Fabregas.

Wang alielezea kwa kupakia picha za pamoja na mchumba wake huku wameshikilia jezi ya Fabregas enzi akiwa Arsenal.

Wachumba hao wanatarajia kufunga pingu za maisha hivi karibuni na walitoa ombi kwa Fabregas wakitaka ahudhurie harusi yao kwani yeye ndiye chanzo na kielelezo kikubwa cha kupendana kwao.

“Mimi ni Yueren, shabiki wako kichaa wa miaka 16 kutoka China. Wewe ndio sababu nilianza kutazama mpira wa miguu. Bado nakumbuka nyakati za usiku za shule yangu ya upili nilikuwa nikisikiliza redio moja kwa moja ya Arsenal (hatukuwa sauti ya TV ya moja kwa moja kwa Ligi ya Premia),” Yuaren aliandika.

Alitoa ombi kwake kumtaka ahudhurie harusi yao na kuwapa baraka kwa sababu mapenzi yao yaliota kwa sababu yake.

“Miaka michache iliyopita, nilikutana na msichana kwa bahati mbaya, na nilifurahi sana kupata kwamba yeye pia ni shabiki wako wazimu kutoka 2010. Hata aliandika maneno ya kupendeza kwako na kuituma kwa Arsenal lakini kwa namna fulani hakujibu alipokuwa mdogo. Upendo wa pande zote wa Fabregas ulituongoza kukusanyika pamoja. Naomba baraka zako kwenye ndoa yetu. Mimi na mke wangu tunapendana kwa sababu yako!” Yuaren alisema.