Historia: Kombe la dunia Qatar kufanyika bila uwepo wa malkia Elizabeth II duniani kwa mara ya kwanza

malkia Elizabeth alizaliwa waka 1926 na mashindano ya kwanza ya kombe la dunia kufanyika 1930.

Muhtasari

• Malkia huyo alishuhudia ushindi wa Uingereza katika kombe la dunia 1966 ambapo Uingereza ilitawazwa mabingwa.

Malkia Elizabeth akimkabidhi kapteni wa Uingereza taji la kombe la dunia 1966
Malkia Elizabeth akimkabidhi kapteni wa Uingereza taji la kombe la dunia 1966
Image: FIFA WORLD CUP//FACEBOOK

Kwa mara ya kwanza katika historia ya kipute kikubwa zaidi duniani, Kombe la dunia, mashindano hayo sasa yatafanyika pasi na uwepo wa malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza.

Itakumbukwa kwamba malkia Elizabeth wa pili ni kama wanarika na kipute hicho kwani anakishinda kwa miaka 4 tu.

Malkia Elizabeth wa pili alizaliwa mwaka 1926 na miaka minne baadae kwa maana ya mwaka 1930, mashindano ya kombe la dunia yakaasisiwa na kuzaliwa.

Mashindano hayo ya kwanza yalifanyika nchini Urugay. Taifa la kwanza kufunga bao katika mashindani hayo lilikuwa ni Ufaransa na wenyeji wa kipute hicho Urugay walikuwa timu ya kwanza kabisa kuwahi kushinda kombe hilo linalotajwa kuwa taji kubwa zaidi duniani katika historia ya mchezo wa kandanda.

Kwa hiyo ni sahihi kusema kwamba tangu kuwepo kwa malkia Elizabeth wa pili duniani, kumekuwepo na kipute cha kombe la dunia kila baada ya miaka minne, na mashindano ya mwaka huu yatakayofanyika nchini Qatar yatakuwa ya kwanza kufanyika bila uwepo wa malkia Elizabeth wa pili.

Baada ya kuapishwa rasmi kama malkia wa Uingereza mwaka 1953 akiwa na umri mbichi, malkia huyo alikuwepo katika ushindi wa pekee wa timu ya taifa ya Uingereza mwaka 1966 ilipotwaa taji la kombe la dunia, ambalo limebakia kuwa la pekee kwa taifa hilo hadi sasa.

Ushindi huo wa Uingereza ulikuwa wa mabao 4 kwa mawili dhidi ya German Magharibi na kuwawezesha kutawazwa kuwa mabingwa wa dunia.

Buriani Malkia Elizabeth wa pili, ama kweli historia huandikwa kwa kufutwa!