NDOVU WAWILI KUMENYANA

Arsenal na Liverpool kupimana nguvu uwanja wa Emirates

Mashabiki wa soka wameshindwa kutabiri atakaye ibuka mshindi.

Muhtasari

•Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta, alisema watakuwa wakikabiliana na timu ambayo ina historia nzuri katika mashindano hayo.

•Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alimsifu Arteta kwa kuwaonyesha wale waliokuwa wakimkosoa hapo awali kwamba ana uwezo wa kuisimamia timu.

Wachezaji wa Arsenal based ya kipenga cha muda wote dhidi ya Manchester City.
Wachezaji wa Arsenal based ya kipenga cha muda wote dhidi ya Manchester City.
Image: John Walton/PA

Kocha mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta, ametabiri ushindani mkali kutoka kwa Liverpool katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili.

Katika mahojiano na vyombo vya habari, Arteta alisema watakuwa wakikabiliana na timu ambayo ina historia nzuri katika mashindano hayo.

"Liverpool ni timu nzuri sana. Ni mechi ambayo kila mtu anaitafuta, dhidi ya mpinzani ambaye ameonyesha katika kipindi cha miaka mitano au sita kiwango alichonacho. Na inabidi tuwaonyeshe wapinzani tena kwamba tumefikia kiwango na tuko tayari kushindana dhidi yao," Arteta alisema."

“Siko hapa kuhukumu Liverpool. Niko hapa kuzungumza juu ya kile tunachofanya. Nafikiri kile ambacho wamefanya katika miaka mitano iliyopita hakihitaji uwasilishaji wowote - ni wazi.

"Wamekuwepo katika kila shindano moja kwa miaka mitano iliyopita, hivyo sifa kwao," aliongeza.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alimsifu Arteta kwa kuwaonyesha wale waliokuwa wakimkosoa hapo awali kwamba ana uwezo wa kuisimamia timu.

"Heshima yangu yote. Kweli, kazi nzuri sana. Unapohitaji muda, hakuna mtu anataka kukupa muda na labda si sote tunastahili muda, kwa sababu bado unapaswa kuwa mzuri katika kutumia muda, na huyo ni Mikel. Lazima niseme, ninamheshimu sana," Klopp alisema.

Kocha huyo alisema watakuwa wakikabiliana na kikosi cha vijana, kilichojaa uwezo.

"Wamekuwa na vipaji vingi katika miaka michache iliyopita. Mstari wa nyuma sasa umetulia, wamepata njia jinsi wanavyotaka kulinda. Ni timu changa, timu ya kusisimua sana, inayofanya vizuri sana na wako katika nafasi wanayostahili.

"Sasa twende huko. Ni wazi hatufikirii kuhusu mechi tulizocheza dhidi yao msimu uliopita kwa sababu haijalishi. Tutajaribu kuwasababishia matatizo, nadhani hiyo ina maana. Kwa hivyo, ninaisubiri kwa hamu," Klopp alisema.

Timu ya Arsenal italenga kubadilisha rekodi yao mbaya ya hivi majuzi dhidi ya Liverpool.

Arsenal wameshinda mchezo mmoja tu kati ya 14 za Premier League dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp. Hata hivyo, wana pointi 11 mbele ya wapinzani wao baada ya kuanza vyema msimu huu.

Arsenal itawakosa Emile Smith Rowe na Mohamed Elneny baada ya kurejea mazoezini na kuwekwa benchi katikati ya wiki.

Ibrahima Konate huenda akacheza mechi yake ya kwanza baada ya kuanza vibaya msimu huu kufuatia jeraha alilolipata kabla ya msimu mpya.