Rapa Drake apoteza milioni 73.3 kufuatia ushindi wa Real Madrid

Timu ya Barcelona ilipoteza 3-1 dhidi ya Real Madrid.

Muhtasari

• Rapa huyo wa Kanada aliiunga mkono Barcelona kushinda, na Arsenal kuibuka washindi kutoka kwa pambano lao la Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leeds.

• Ferran Torres aliifungia Barca bao la kufuta machozi, lakini hatimaye, halikumaanisha chochote.

Image: Instagram

Drake alipoteza Pauni 537,000 baada ya kuweka ubashiri kwenye Barcelona ili kuifunga Real Madrid kwenye El Clasico siku ya Jumapili.

Rapa huyo wa Kanada aliiunga mkono Barcelona kushinda, na Arsenal kuibuka washindi kutoka kwa pambano lao la Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leeds.

Alikuwa katika mstari wa kushinda pauni milioni 2.5 ikiwa ubashiri huo ungekuwa mzuri, lakini Real Madrid walipata ushindi wa 3-1 kwenye uwanja wa Bernabeu.

Ikiwa wote wawili wangeibuka washindi, angeshinda Euro milioni 2.89. (Ksh 341,019,373.45)

Ushindi wa Real Madrid ulifanya meneja wa klabu hiyo Carlo Ancelotti kudai kwamba anajivunia El Clasico ambayo ilikuwa ya kwanza  msimu huu ambako waliandikisha ushindi wa 3-1 dhidi ya wababe hao wa Barcelona.

Mabao ya washambulizi Karim Benzema, Federico Valverde, na Rodrygo yalitosha kuvuna ushindi huku Real Madrid wakisonga hadi nafasi ya kwanza katika jedwali la La Liga.

Ferran Torres aliifungia Barca bao la kufuta machozi, lakini hatimaye, halikumaanisha chochote.

 Drake alikuwa akisherehekewa na klabu ya Barcelona katika mechi hiyo ya  El Clasico kwa sababu ya kuwa msanii wa kwanza kuwa na mashabiki zaidi ya  Bilioni hamsini  kwenye mtandao wa Spotify.

 Kufuatia hilo, wachezaji wa Barcelona walikuwa wamevaa jezi maalum zenye nebo ya bundi kwa ajili ya supastaa huyo.