Ballon d'Or: Karim Benzema ashinda tuzo ya mchezaji bora wa soka duniani kwa mara ya kwanza

Alexia Putellas wa Barcelona alihifadhi tuzo ya Ballon d'Or ya Wanawake

Muhtasari

•Benzema alifunga mabao 44 katika michezo 46 alipoisaidia Real kushinda Ligi ya Mabingwa na La Liga msimu wa 2021-22.

Karim Benzema akikabidhiwa tuzo hiyo na Zinedine Zidane
Image: BBC

Mshambuliaji wa Real Madrid na Ufaransa Karim Benzema ameshinda tuzo ya Ballon d'Or - tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka huu - kwa mara ya kwanza.

Benzema alifunga mabao 44 katika michezo 46 alipoisaidia Real kushinda Ligi ya Mabingwa na La Liga msimu wa 2021-22.

Lionel Messi (saba) na Cristiano Ronaldo (tano) walikuwa wameshinda tuzo hiyo mara 12 kati ya 13 zilizopita.

Sadio Mane wa Bayern Munich, ambaye alikuwa Liverpool msimu wa 2021-22, alikuwa wa pili mbele ya Kevin de Bruyne wa Manchester City.

Alexia Putellas wa Barcelona alihifadhi tuzo ya Ballon d'Or ya Wanawake, iliyotolewa kwa mwanasoka bora wa kike wa 2022.

Mshindi wa England Euro 2022 na mshambuliaji wa Arsenal Beth Mead alikuwa wa pili.

Mabingwa wa Premier League Manchester City, ambao walikuwa na wachezaji  sita walioteuliwa  kwenye sherehe hizo, walitunukiwa Klabu Bora ya Mwaka mbele ya Liverpool.

Tuzo ya Ballon d'Or hutunukiwa mwanasoka bora wa mwaka, kulingana na utendaji wake katika msimu wa 2021-22.

Matokeo ya Ballon d'Or

1. Karim Benzema (Real Madrid, France).

2. Sadio Mane (Bayern Munich, Senegal).

3. Kevin de Bruyne (Manchester City, Belgium).

4. Robert Lewandowski (Barcelona, Poland).

5. Mohamed Salah (Liverpool, Egypt).

6. Kylian Mbappe (Paris St-Germain, France).

7. Thibaut Courtois (Real Madrid, Belgium).

8. Vinicius Junior (Real Madrid, Brazil).

9. Luka Modric (Real Madrid, Croatia).

10. Erling Haaland (Manchester City, Norway).

11. Son Heung-min (Tottenham Hotspur, South Korea)

12. Riyad Mahrez (Manchester City, Algeria).

13. Sebastien Haller (Borussia Dortmund, Ivory Coast).

14. Fabinho (Liverpool, Brazil) alikuwa sawa na Rafael Leao (AC Milan, Portugal).

16. Virgil van Dijk (Liverpool, Netherlands).

17. Luis Diaz (Liverpool, Colombia) alikuwa sawa na Dusan Vlahovic (Juventus, Serbia) na Casemiro (Manchester United, Brazil).

20. Cristiano Ronaldo (Manchester United, Portugal).

21. Harry Kane (Tottenham Hotspur, England).

22. Trent Alexander-Arnold (Liverpool, England) alikuwa nafasi sawa na Phil Foden (Manchester City, England) na Bernardo Silva (Manchester City, Portugal).

25. Joao Cancelo (Manchester City, Portugal) alikuwa sawa na Joshua Kimmich (Bayern Munich, Germany), Mike Maignan (AC Milan, France), Antonio Rudiger (Real Madrid, Germany), Darwin Nunez (Liverpool, Uruguay) na Christopher Nkunku (RB Leipzig, France).