Ten Hag amrudisha Ronaldo kwenye kikosi cha kwanza baada ya kumfungia nje kwa muda

Kiungo mshambuliaji huyo Mreno alifungiwa nje wiki moja baada ya kukataa kuingia uwanjani kama mchezaji wa akiba kunako dakika ya 89.

Muhtasari

• Ten Hag na Ronaldo wamefanya mazungumzo tangu tukio hilo wiki iliyopita na meneja alifurahi kumkaribisha Ronaldo kikosini baada ya majadiliano hayo.

Ten Hag akinong'onezana na Ronaldo
Ten Hag akinong'onezana na Ronaldo
Image: The Guardina

Kiungo mshambulizi wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amerejea kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, akijiunga na kundi hilo mazoezini kuelekea mechi yao ya nyumbani ya UEFA Europa League dhidi ya Sheriff Tiraspol kutoka Moldova.

Nyota huyo wa zamani wa klabu hiyo mwenye umri wa miaka 37 aliagizwa kufanya mazoezi peke yake wiki jana na meneja Erik ten Hag baada ya kukataa kuingia kama mchezaji wa akiba katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Tottenham Jumatano iliyopita.

Hatimaye aliondolewa katika ziara ya Mashetani Wekundu uwanjani Stamford Bridge Jumamosi, ambapo walitoka sare ya 1-1 na Chelsea.

Ronaldo alilaumu "joto la wakati huu" baada ya kuondoka Old Trafford kabla ya mwisho wa ushindi wa 2-0 wa United dhidi ya Spurs, baada ya kuondoka kwenye benchi na kushuka kwenye njia ya kuelekea nje ya uga kunako dakika ya 89.

Kushiriki kwa Mreno huyo katika mazoezi kunapendekeza kwamba huenda akachaguliwa kucheza dhidi Sheriff Tiraspol siku ya Alhamisi katika mpambano wa Kundi E wa Ligi ya Europa.

Tangu sare ya 1-1 na Chelsea Jumamosi, wachezaji wa United wamekuwa na siku mbili za mapumziko hivyo walirejea Carrington Jumanne kuanza maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Europa dhidi ya Sherrif Tiraspol, utakaofanyika Alhamisi.

Ten Hag na Ronaldo wamefanya mazungumzo tangu tukio hilo wiki iliyopita na meneja alifurahi kumkaribisha Ronaldo kikosini baada ya majadiliano hayo.

Ten Hag alitaka kujua Ronaldo alikuwa amejitolea kwa mradi wake kabla ya kumkaribisha mchezaji huyo, lakini sasa amepata uhakikisho wa kutosha kumrejesha kundini kwa mara ya kwanza.