CR7: Kutoka kuonewa na kudharauliwa uwanjani hadi kuwa staa mkubwa

Mara moja alikasirika sana alipohisi mwalimu alikuwa akitania jinsi anavyozungumza, akamrushia kiti.

Muhtasari

• Kulingana na The Sun, alisajiliwa na Sporting akiwa na umri wa miaka 12 lakini miaka yake ya kwanza ilikuwa migumu sana.

Ronaldo enzi ya zamani na sasa
Ronaldo enzi ya zamani na sasa
Image: Instagram, Gatty Images

“Christiano Ronaldo alifikiria kuacha soka kabla ya kupata mwanya mkubwa maishani mwake alipojiunga na Manchester United kutokana na uonevu wa mara kwa mara, upweke na kutamani nyumbani,” The Sun wanaripoti.

Kulingana na jarida hilo ambalo limenukuu wasifu ambao umeandikwa kwa jina Messi vs Ronaldo: One Rivalry, Two GOATs mchezaji huyo ingawa sasa ni mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia, Ronaldo alilazimika kushinda shida kubwa wakati wa siku zake katika akademi ya Sporting Lisbon.

Kitabu hicho kinadai nyota huyo wa Mashetani Wekundu - ambaye alishinda mataji matano ya Ligi ya Mabingwa na tano za Ballon d'Or - nusura ajikatae kutoka kwa masuala ya soka huku akihangaika kupatana na watoto wenzake mazoezini.

Ronaldo alizaliwa Februari 1985 kwenye kisiwa cha Madeira - maili 535 kutoka mji mkuu wa Ureno Lisbon.

Kulingana na The Sun, alisajiliwa na Sporting akiwa na umri wa miaka 12 lakini miaka yake ya kwanza ilikuwa migumu sana hivi kwamba kitabu kipya kilichochapishwa wiki hii kinadai Ronaldo:

  • Alitaniwa bila huruma kwa lafudhi yake nzito ya Madeiran na wavulana wengine.
  • Alijikuta katika mfululizo wa matukio ya milipuko na mikwaruzo kwenye uwanja wa shule.
  • Mara moja alikasirika sana alipohisi mwalimu alikuwa akitania jinsi anavyozungumza, akamrushia kiti.
  • Alilia kila siku kwa miezi huku akiikosa familia yake na marafiki wa eneo hilo.
Messi, Ronaldo
Messi, Ronaldo

Jarida hilo linazidi kueleza kwamba mchezaji huyo alikuwa na uhakika wa kuwa bora katika malimwengu ya soka na alikuwa anawaambia marafiki zake.