Kila nilipogusa mpira walikuwa wakifanya kelele za tumbili"-Victor Wanyama

Wanyama anasema mengi yanahitaji kufanyika barani ulaya ili kukomesha ubaguzi katika soka.

Muhtasari

• Wanyama alitoa mfano wa jinsi mashabiki walivyokuwa wakitoa sauti kama za nyani katika mechi moja wakiwa nchini Urusi.

• Nyota huyo alisema..."Wakati mwingine hainusumbui lakini ni jambo baya, wakati mwingine nikiwa peke yangu kisha nifikirie kilichotokea ndipo napoona ilikuwa vibaya".

Image: BBC

Nyota wa soka wa Kenya Victor Wanyama na aliyewahi kuichezea Tottenham Hotspurs amesimulia jinsi alivyowahi kukumbana na ubaguzi wa rangi katika soka akiwa barani Ulaya.

Wanyama ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya CF Montreal nchini Canada amesema visa kama hivyo vya ubaguzi wa rangi sio mfano mzuri kwa soka.

Akizungumza katika mahojiano na BBC mchezaji huyo alitoa mfano wa jinsi mashabiki walivyokuwa wakitoa sauti kama za nyani katika mechi moja wakiwa nchini Urusi.

"Wakati mwingine hainusumbuilakini ni jambo baya ,wakati mwingine nikiwa peke yangu kisha nifikirie kilichotokea ndipo napoona ilikuwa vibaya".

Wanyama anasema mengi yanahitaji kufanyika barani ulaya ili kukomesha ubaguzi katika soka.

‘wanaonya hivyo wanafaa kupigwa faini kubwa au wapigwe marufuku kutoka soka’ anasema

Kuhusu pendekezo la baadhi ya vilabu kusema kwamba havitawasajili wachezaji waafrika kwa sababu wanahitajika wakati mwingine kuziwakilisha nchi zao,Wanyama anasema panafaa kuwa na heshima kwa nchi hizo za kiafrika.

Nyota huyo maajuzi alikuwa Spurs lakini anasema alikwenda kuwajulia hali wenzake wa zamani na hana mpango wa kurejea katika klabu hiyo .