Hazard: Siwezi eleza kwa nini nikiwa Chelsea sikuwa napata majeraha kama Madrid

Mashabiki wa Madrid, nisameheni jamani. Si rahisi kuwa huwa sichezi kila mara - Hazard.

Muhtasari

• Pia aliwaomba msamaha mashabiki wake wa Madrid ambao wangependa kumuona akicheza ila imekuwa tofauti kutokana na majeraha.

Mchezaji wa Ubelgiji, Eden Hazard
Mchezaji wa Ubelgiji, Eden Hazard
Image: Instagram

Mchezaji kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji na miamba wa soka wa Uhispania Realc Madrid, Eden Hazard amezungumzia kuhusu maisha yake ya changamoto nyingi katika klabu hiyo.

Katika mazungumzo ya kipekee na jarida la Marca, Hazard alianza kwa kuwaomba msamaha mashabiki wake wengi wanaoishabikia Madrid kwa sababu yake na kusema yeye muda wote ana ari na uchu wa kuitumikia timu uwanjani lakini majeraha yamekuwa sehemu ya maisha yake.

Alizidi kusema kuwa hata yeye akiulizwa hawezi kuwa na maelezo kamili kuhusu msururu wa majeraha ambayo yamekuwa yakimwandama tangu mwaka 2018 alipoigura Chelsea kwenda Real Madrid.

Alisema kuwa akiwa Chelsea alikuwa anacheza mechi nyingi tu bila jeraha lakini Madrid imekuwa ni tofauti kwani majeraha yamemweka nje na kumharibia tasnia yake ya usakataji kandanda.

“Mashabiki wa Madrid, nisameheni jamani. Si rahisi kuwa huwa sichezi kila mara. Huwa nataka kucheza muda wote lakini ninaomba radhi kwa kile kinachotokea. Nikiwa Chelsea, nilicheza mamia ya mechi bila majeraha. Lakini huku Madrid, nimekuwa nikirundikwa na majeraha, ni kitu amabcho siwezi kuwa na maelezo pia,” Hazard alisema.

Staa huyo kwa kupiga chenga za kimaudhi aliisakatia Chelsea mechi 352 na kufunga mabao 110 ndani ya miaka 7 ambayo alitumikia miamba hao wa Uingereza.

Akiwa Madrid, tangu mwaka 2019 mpaka sasa, ameshiriki mechi chache mno kulinganishwa na muda ule ambao amedumu klabuni hapo.

Tetesi za soka zimekuwa zikiakisi kuwa kocha wa Madrid amemwambia kutafuta klabu nyingine ya kumsajili kwa sababu nafasi yake klabuni hapo haionekani kuendelea kuwepo.