Makontena ya mashabiki Qatar kutolewa kama msaada kwa wasio na makazi Kenya - China

Naibu waziri wa masuala ya nje wa China alitangaza kupitia Tweeter yake. Makonteina hayo yanatumika kama makazi ya mashabiki wa kombe la dunia Qatar.

Muhtasari

• Kontena moja lina uwezo wa kuwahudumia watu wawili na makonteina yenyewe ni takribani lefu 6.

Makonteina ya mashabiki
Makonteina ya mashabiki
Image: Getty Images

Nchi ya Kenya inatarajiwa kufaidika pakubwa pindi tu mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini Qatar yatakamilika kati mwa mwezi Desemba.

China imetangaza kuwa vyumba vya kuhamishwa ambavyo vinatumika kama makaazi ya mashabiki wanaohudhuria kombe la dunia nchini Qatar vitatolewa kama msaada kwa watu wasiokuwa na makazi nchini Kenya mwishoni mwa mashindano hayo mwezi kesho.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, jamaa aliyetajwa kama naibu waziri wa masuala ya kigeni wa Uchina Hua Chunying alitangaza kuwa vyumba hivyo vya kuhamishwa maarufu ‘Cabin’ kwa lugha ya kimombo ni zaidi ya elfu 6 na kila kimoja kina uwezo wa kumudu watu wawili ndani.

“Vyumba hivyo vya mashabiki 6,000 vinavyokaa kama kijiji katika mashindano ya FIFAWorldCup. Majumba hayo yalitengenezwa na makampuni ya China, na yatatolewa kwa watu wasio na makazi nchini Kenya baada ya michezo hiyo,” naibu waziri huyo alisema.

Kando na uwezo wa kuwamudu watu wawili, Makabati hayo yana huduma kama friji, bafuni, huduma za utunzaji wa nyumba na unganisho la mtandao.

Lakini baada ya waziri huyo kutangaza hivyo, watu mbalimbali walitoa maoni yao huku wengine wakisema kuwa hatua hiyo haitasuluhisha tatizo la watu wasio na makazi nchini na wengine wakisema kuwa Kenya haikufaa kupewa msaada huo.

“Nzuri lakini moto sana. Niliona vyumba vikiwa na vipozezi vya kinamasi, ambavyo hufanya kazi vizuri katika hali ya hewa kavu ya joto lakini havina maana nchini Kenya, ambako hali ya hewa ni ya unyevunyevu mwaka mzima. Afadhali kuzituma kwa nchi za Sahara/Sahel. Bila kibanda cha baridi cha majani au hema ni vizuri zaidi kuliko kibanda kilichofungwa nchini Kenya.” Mmoja kwa jina Paula Paalu aliandika.