Senegal 'haijashindwa’ katika Kombe la dunia– Rais Macky

Lions of Teranga walifungwa 3-0 na England katika awamu ya mchujo.

Muhtasari

•Senegal hawakuwa na wachezaji wao muhimu jambo ambalo lililodhihirisha pigo kwao wakati safu ya kati ilipotawaliwa na wachezaji wa England.

Kombe la Dunia
Image: GETTY IMAGES

Ulikuwa ni usiku wa kukata tamaa kwa Senegal katika Kombe la dunia nchini Qatar Jumapili baada ya kufungwa 3-0 na England katika awamu ya mchujo.

Teranga Lions hawakuwa na wachezaji wao muhimu jambo ambalo lililodhihirisha pigo kwao wakati safu ya kati ilipotawaliwa na wachezaji wa England.

England itakutana na Ufaransa katika robo fainali siku ya Jumamosi.

Katika ujumbe wa Twitter, Rais wa Senegal Macky Sall alielezea kutoridhishwa kwake na mchezo wa timu katika mashindano hayo.

Alisema: "Wapendwa Lions (Simba), Hamjashindwa. Na mlicheza bila Sadio [Mane], [Cheikhou] Kouyate na [Idrissa] Gana.

Mko miongoni mwa timu 16 bora duniani na England walikuwa wapinzani imara."

Talisman Sadio Mane alielezea hisia sawa na hizo kwenye Twitter.

"Watu wanajivunia sana safari yenu ambao imefurahisha mioyo ya mashabiki wenu, kulinda benderakwa heshima."

Aliongeza kusema kuwa: "Kujifunza kunaendelea. Tutatafuta vikombe vingine .":