Kombe la Dunia 22:Kombe la Dunia limekuwa bora zaidi kuwahi kushuhudiwa - Infantino

"Hadi dakika ya mwisho ya mechi ya mwisho usingejua ni timu gani itaendelea'', anasema Infantino.

Muhtasari
  • Infantino amesema kwamba hilo litaangaliwa baada ya "mafanikio " ya makundi ya timu nne katika Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar

Mkuu wa shirikisho la Soka Duniani Gianni Infantino amesema Kombe la Dunia la mwaka huu linalofanyika nchini Qatar ni bora zaidi kuliko mashindano ya aina hiyo yaliyowahi kufanyika katika historia yake.

Bw Infantino Infantino alikuwa akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari nchini Qatar, baada ya kuhudhuria mkutano wa baraza la Fifa.

Huku zikisalia mechi za kutafuta mshindi wa tatu na fainali , mkuu huyo wa Fifa anasema kuwa mashabikii 3.27 ndio waliohudhuria mechi ikilinganishwa mashabiki milioni 3.3 waliohudhuria katika Kombe la dunia la Urusi mwaka 2018 kwa ujumla.

"Asante kwa kila mmoja aliyehusika, Qatar, wale wote walijitolea kulifanya Kombe hili la Dunia kuwa bora zaidi kuwahi kushuhudiwa ," alisema Infantino.

"Mechi zimechezwa bila matukio. Kumekuwa na hali ya furaha sana’’

"Kuna kitu kinachotokea tunapozungumzia kuhusu soka kuwa mchezo halisi wa dunia, huku timu ya Afrika [Morocco] ikifika robo fainali kwa mara ya kwanza.

Fifa kuangalia upya mpangilio wake katika Kombe la Dunia la 2026

Wakati huo huo rais huyo wa Fifa amesema shirikisho hilo la soka duniani litaangalia upya mpangilio wake katika Kombe la Dunia la 2026 Marekani,Mexico na Canada.

Timu zitaongezeka kutoka 32 hadi 48 kwa ajili ya shindano hilo, na zinapangwa kugawanywa katika makundi 16 ya timu tatu, ambapo timu mbili zitakazoongoza katika kundi zitaweza kuendelea na kuingia katika 32 za mwisho.

Infantino amesema kwamba hilo litaangaliwa baada ya "mafanikio " ya makundi ya timu nne katika Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.

"Hapa makundi ya timu nne yamekuwa Here the groups of four have been absolutely mazuri ajabu," alisema Infantino.

"Hadi dakika ya mwisho ya mechi ya mwisho usingejua ni timu gani itaendelea'', anasema Infantino.